عَنْ أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيّ رضى الله عنه، قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اللهِ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ، فَقَالَ: «إِنَّ اللهَ - عزَّ وجلَّ - لَا يَنَامُ،  « وَلَا يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ، يَخْفِضُ الْقِسْطَ وَيَرْفَعُهُ، يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ، وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ، حِجَابُهُ النُّورُ - وَفِي رِوَايَةٍ: النَّارُ - لَوْ كَشَفَهُ لَأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ».

Kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ariy, (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisimama na kutueleza mambo matano, akasema:“Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mtukufu, halali usingizi.Wala hahitajii kulala,Anashusha mizani na kuinyanya.Matendo yote yanayo tendeka usiku hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya mchana, na Matendo yote yanayo tendeka mchana hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya usiku.Kizuizi (kati yake na viumbe wake) ni Nuru - na katika riwaya: Moto.Akiondoa kizuizi hicho, Utukufu wa uso wake utachoma kila kiumbe ataefikiwa na macho yake katika viumbe wake”

Related by Muslim, 179.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Mwenyezi Mungu - hapana Mwenyezi mungu anaeabudiwa kwa haki ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala”

[Al-Baqarah: 255].

Na Amesema pia Mwenyezi Mungu

 “Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu (10) Waandishi wenye hishima na utukufu (11) Wanayajua mnayo yatenda”

[Al Infitar: 10 - 12].


Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

“Kwake Yeye hupanda neno zuri, na Matendo mema yeye huyatukuza”

[Fatir: 10].


Mwenyezi Mungu Amesema:

“Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbinguni na Ardhini. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa yenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu”

[An-Nur: 35].

Miradi ya Hadithi