عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ قَالَ: «إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا؛ مِائَةً إِلَّا وَاحِدًا، مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الجَنَّةَ»، زَادَ في رواية: «إِنَّهُ وِتْرٌ يُحِبُّ الْوِتْرَ». متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) Amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa.mia moja ispokuwa moja,Mwenye kuyadhibiti ataingia Peponi.”Akaongeza katika riwaya nyingine: “hakika yeye (Mwenyezi Mungu) ni witiri anapenda witiri.”

imepokelewa na Bukhari Na Muslim

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 ﴾Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda﴿.

[Al-A'raf: 180].

Na Amesema Pia:

﴾Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo﴿.

[Al-Isra: 110].

Na Amesema Aliyetakasika

﴾22. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.23. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.24. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima﴿

[Al-Hashr: 22 - 24]

Miradi ya Hadithi