عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما، أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ، قَالَ: «بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما، أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ، قَالَ: «بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
Kutoka kwa Abdullah bin Amr, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema:
1- “Fikisha kwa niaba yangu hata ikiwa ni Aya.
2- Na simulieni kwa niaba ya Wana wa Israili, wala hakuna ubaya ndani yake.
3- Na mwenye kunisingizia uwongo kwa makusudi basi na ajiandalie makao yake Motoni.”
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ujuzi - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina”.
[Yusuf: 108]
Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa”.
[An-Nahl: 116]
Na akasema Mwenyezi Mungu:
“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka” .
[An-Nahl: 125]
Na Amesema Mwenyezi Mungu:
“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu” .
[Fussilat: 33]