19 - KUMPENDA MTUME NA YANAYOFUNGAMANA NA HAYO

عَن أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضى الله عنه، قَالَ: بَيْنَمَا أَنَا وَالنَّبِيُّ ﷺ خَارِجَانِ مِنَ المَسْجِدِ، فَلَقِيَنَا رَجُلٌ عِنْدَ سُدَّةِ المَسْجِدِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «مَا أَعْدَدْتَ لَهَا؟»، فَكَأَنَّ الرَّجُلَ اسْتَكَانَ، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا أَعْدَدْتُ لَهَا كَبِيرَ صِيَامٍ، وَلا صَلاةٍ، وَلا صَدَقَةٍ،وَلَكِنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ، قَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». 


Kutoka kwa Anas bin Malik (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

Wakati mimi na Mtume (Rehma na Amani zimshukie) tunatoka msikitini tulikutana na mtu mmoja kwenye uwanja wa msikiti, (sehemu ya mbele) akasema (yule mtu): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Qiyama ni lini?Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akasema: “Umeandaa nini kwa ajili yake?”Mtu alikuwa huyo kana kwamba amekata tamaa.akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijajiandaa kwa funga nyingi, swala, wala sadaka.Lakini mimi nampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.Akasema Mtume (Rehma na Amani zimshukie): «Wewe utakuwa pamoja na uwapendao (siku ya kiama)

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

“Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari”

[Luqman: 34].

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

 “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu”

[Al Imran: 31].

Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapo pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao”

[An-Nisa: 69].

Amesema Mtukufu

“Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu”

[Alt-Toba: 24]

Miradi ya Hadithi