19 - KUMPENDA MTUME NA YANAYOFUNGAMANA NA HAYO

عَن أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضى الله عنه، قَالَ: بَيْنَمَا أَنَا وَالنَّبِيُّ ﷺ خَارِجَانِ مِنَ المَسْجِدِ، فَلَقِيَنَا رَجُلٌ عِنْدَ سُدَّةِ المَسْجِدِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «مَا أَعْدَدْتَ لَهَا؟»، فَكَأَنَّ الرَّجُلَ اسْتَكَانَ، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا أَعْدَدْتُ لَهَا كَبِيرَ صِيَامٍ، وَلا صَلاةٍ، وَلا صَدَقَةٍ،وَلَكِنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ، قَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». 


Kutoka kwa Anas bin Malik (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

Wakati mimi na Mtume (Rehma na Amani zimshukie) tunatoka msikitini tulikutana na mtu mmoja kwenye uwanja wa msikiti, (sehemu ya mbele) akasema (yule mtu): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Qiyama ni lini?Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akasema: “Umeandaa nini kwa ajili yake?”Mtu alikuwa huyo kana kwamba amekata tamaa.akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijajiandaa kwa funga nyingi, swala, wala sadaka.Lakini mimi nampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.Akasema Mtume (Rehma na Amani zimshukie): «Wewe utakuwa pamoja na uwapendao (siku ya kiama)

Anas bin Malik bin Al-Nadr bin Damdam Al-Ansari

Anas bin Malik bin Al-Nadr bin Damdam Al-Ansari, Abu Hamza, imamu, mufti, msomaji, Mbobezi katika fani ya hadithi, msimuliaji wa Uislamu, Mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yake, na wa mwisho kufa katika masahaba huko Basra. Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuja Madina akiwa na umri wa miaka kumi, na wakati Mtume anakufa Anasi alikuwa na umri wa miaka ishirini, na alikuwa akimtumikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake. Alishiriki vita pamoja na Mtume zaidi ya mara moja, na alimpa ahadi ya utii chini ya mti. Alipokea kutoka kwa Mtume elimu kubwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake alimwombea dua ya mali nyingi na watoto, na shamba lake la mitende lilikuwa likipamba mara mbili kwa mwaka, alifariki mwaka: (93 AH) [1]


Marejeo

1.  Rejea ufafanuzi wake katika: “Sir Al-Alam Al-Nubala” cha Al-Dhahabi (4/417-423), “Ma`rifat Al-Sahaba” cha Abu Naim (1/231), “Kamusi ya Maswahaba. ” cha Al-Baghawi (1/43), “Asad Al-Ghaba” cha Ibn Al-Atheer (1/ 151-153).

Miradi ya Hadithi