19 - KUMPENDA MTUME NA YANAYOFUNGAMANA NA HAYO

عَن أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضى الله عنه، قَالَ: بَيْنَمَا أَنَا وَالنَّبِيُّ ﷺ خَارِجَانِ مِنَ المَسْجِدِ، فَلَقِيَنَا رَجُلٌ عِنْدَ سُدَّةِ المَسْجِدِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «مَا أَعْدَدْتَ لَهَا؟»، فَكَأَنَّ الرَّجُلَ اسْتَكَانَ، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا أَعْدَدْتُ لَهَا كَبِيرَ صِيَامٍ، وَلا صَلاةٍ، وَلا صَدَقَةٍ،وَلَكِنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ، قَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». 


Kutoka kwa Anas bin Malik (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

Wakati mimi na Mtume (Rehma na Amani zimshukie) tunatoka msikitini tulikutana na mtu mmoja kwenye uwanja wa msikiti, (sehemu ya mbele) akasema (yule mtu): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Qiyama ni lini?Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akasema: “Umeandaa nini kwa ajili yake?”Mtu alikuwa huyo kana kwamba amekata tamaa.akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijajiandaa kwa funga nyingi, swala, wala sadaka.Lakini mimi nampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.Akasema Mtume (Rehma na Amani zimshukie): «Wewe utakuwa pamoja na uwapendao (siku ya kiama)

Muhtasari wa Maana

Swahaba mmoja alimuuliza Mtume (Rehma na Amani zimshukie) kuhusu lini kitasimama Kiyama, Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akamuuliza kwanza yale ambayo ni muhimu zaidi kuliko kujua wakati wake nayo ni maandalizi yake. mtu yule akasema kuwa hakutayarisha matendo mengi, isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akamwambia kwamba hii ni sababu ya kuingia Peponi, na kuwa karibu nae huko, ikiwa atakuwa na nia thabiti katika mapenzi yao.

Miradi ya Hadithi