عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ، فَسَأَلَهُ عَنْ أَشْرِبَةٍ تُصْنَعُ بِهَا، فَقَالَ: «وَمَا هِيَ؟» قَالَ: البِتْعُ وَالْمِزْرُ، فَقُلْتُ لِأَبِي بُرْدَةَ: مَا البِتْعُ؟ قَالَ: نَبِيذُ العَسَلِ، وَالْمِزْرُ نَبِيذُ الشَّعِيرِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ»

Kutoka kwa Said bin Abi Burdah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi nao, 1. Mtume rehma na Amani zimshukie alimtuma Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyotengenezwa huko, akasema: “Ni nini? Akasema: Al-bit’u na Al-mizru, basi nikamwambia baba Burdah: Al-bit’u ndio nini? Akasema: mchanganyo wa asali, na Al-mizru, ni mchanganyo wa shayiri. 2. Akasema: “Kila kilevi ni haramu”

 


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa (90) Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha”

[Al-Ma’idah: 90, 91]

Miradi ya Hadithi