عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي اللَّه عنهمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «مَا زَالَ جِبْرِيلُ يُوصِينِي بِالْجَارِ، حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ»
عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي اللَّه عنهمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «مَا زَالَ جِبْرِيلُ يُوصِينِي بِالْجَارِ، حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ»
Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema:
Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema: “Jibril alikuwa akiniusia kuhusu jirani mpaka nikadhania kuwa atakuwa miongoni mwa warithi
Jibril Rehema na Amani zimshukie akazidi kumshukia Mtume Rehema na Amani zimshukie, akimwagiza kumfanyia wema jirani, kuhifadhi haki zake, kumuepusha na madhara, kushiriki furaha naye, na kumliwaza wakati wa huzuni, na kupeana zawadi na sadaka, Na kumfanyia wema kwa kauli na vitendo, na mengineyo yanayo onyesha kumkirimu jirani, mpaka Mtume Rehema na Amani zimshukie akafikiri kwamba wahyi utateremshwa kuwa jirani anamrithi jirani yake faradhi au taasweb kama livyo mirathi ya ndugu.
Aya za Qur’an zimekuja kumuusia jirani; Mwenyezi Mungu anasema:
“Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri”
[An-Nisa: 36].
Na akaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwamba wema kwa jirani ni miongoni mwa alama za imani, basi akasema Mtume amani iwe juu yake: “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho asimdhuru jirani yake” [1] Na akaapa mara tatu kwamba mwenye kumdhuru jirani yake si Muumini; Akasema rehma na Amani zimshukie: “Wallahi hana imani, Wallahi hana imani, Wallahi hana imani” Ikasemwa: Ni nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ambaye jirani yake hana amani naye” [2] bali hataingia Peponi kwa mujibu wa alivyosema Mtume Rehma na Amani zimshukie: “Hataingia Peponi mtu ambaye jirani yake hapati amani yake” [3]
Jirani wako aina nyingi; kuna Jirani Mwislamu yuko karibu: ana haki ya ujirani na haki ya udugu katika Uislamu na haki ya jamaa, na kuna jirani Mwislamu yuko mbali: ana haki ya ujirani na haki ya udugu katika Uislamu, na jirani kafiri: ana haki ya ujirani tu [4]
1. Mazungumzo mengi juu ya jambo fulani, msikilizaji hupata umuhimu mkubwa na humtia moyo kufanya yale anayotakiwa kufanya, na ndio maana Mtume akarudia maneno yake mara tatu. Hivyo yatakikana kwa Mlinganiaji, Mwalimu, na mwanasheria lazima awe makini na masuala muhimu ya taifa na kuyazungumza mara nyingi katika mikutano na masomo yake.
2. Jirani anayo haki kubwa iliyotajwa na Qur’ani Tukufu na Sunna zilizotakasika za Mtume, hivyo Muislamu lazima aitimize haki hiyo na asiipuuze.
3- Kumuudhi jirani ni dalili ya kukosa imani, na kumheshimu ni sehemu ya imani. Kwa hivyo jiangalie mwenyewe na imani yako, ni kuongeza au kupunguza?
4- Abu al-Jahm al-Adawi aliuza nyumba yake kwa dirham laki moja, na mnunuzi alipokuja kuichukua, Abu al-Jahm akasema: Hii ni bei ya nyumba, basi utanunua kiasi gani ujirani wa Said bin Al-Aas? Akasema: Je, tangu lini ujirani ukanunuliwa?! Akasema: Nirudishie nyumba na uchukue pesa zako, siwezi kuacha ujirani wa mtu ambaye, nikikaa ananiuliza, na akiniona ananikaribisha, na nisipokuwepo ananilinda. na nikiwepo ananiweka karibu, na nikimuomba ananitimizia, Na kama nisipomuomba angenianza, na ikinipata shida, basi ananiondolea. Basi habari zikafika kwa Saiyd, basi Sayd akampelekea dirham laki moja, na akasema: Hii ni bei ya nyumba yako, na nyumba ni yako [5]
5- Ni haki ya jirani juu ya jirani yake kuyavumilia baadhi ya madhara ya jirani yake, na asiwe mwepesi wa kumlalamikia.” Al-Hasan Al-Basri amesema: “Kuwa na ujirani mwema si kuacha madhara, lakini ujirani ni kuvumilia madhara” [6]
6. Mshairi alisema:
Na tunamkirimu jirani yetu maadamu yuko nasi = Na tunamfuata kwa utu popote alipo.
Jirani anakaa nasi muda wote, anapaswa kuogopa kutiwa chumvi.
7. Mwingine akasema:
Wananilaumu kwa kuuza nyumba yangu kwa bei nafuu = na hawakuona jirani pale akipiga kelele.
Basi nikawaambia acheni kulaumu, maana ni kwa majirani nyumba hizo zinazidi kwenda na kuwa nafuu.
1. Imepokewa na Al-Bukhari (6018), na Muslim: (47).
2. Imepokewa na Al-Bukhari (6016).
3.Imepokewa na Muslim (46).
4. "Almifham Lamaa 'Ushakil Min Talkhis Kitab Muslimin" Cha Abu Al-Abbas Al-Qurtubi (1/228), “Al-Ta’iin fi Sharh Al-Arba’iyn” cha Suleiman bin Abdul-Qawi ( 1/136)
5. “Rabi’ al-Abrar” cha al-Zamakhshari (1/393).
6. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab al-Hanbali (1/353).