عن عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ – رضي الله عنه - قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ ﷺ ذَاتَ يَوْمٍ، إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعَرِ، لَا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلَا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ،حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ ﷺ، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «الْإِسْلَامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ ﷺ،وَتُقِيمَ الصَّلَاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ،وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلًا»، قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ، وَيُصَدِّقُهُ،قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِيمَانِ، قَالَ: «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلَائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الْآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ»، قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِحْسَانِ، قَالَ: «أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ»، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ، قَالَ: «مَا الْمَسْؤولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ»قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَتِهَا، قَالَ: «أَنْ تَلِدَ الْأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ»،قَالَ: ثُمَّ انْطَلَقَ فَلَبِثْتُ مَلِيًّا، ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا عُمَرُ أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ». رواه مسلم.



Kutoka kwa Umar bin Al-Khattab – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi –amesimulia kuwa:

siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani ziwe juu yake) ghafla alitokea mtu mwenye mavazi meupe mno, mwenye nywele nyeusi sana, hana athari yoyote safari ndefu, na hakuna kati yetu aliyemfahamu.Alisogea na kukaa karibu na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akiegemeza magoti yake juu ya magoti yake na akaweka mikono kwenye mapaja yake.Kisha akasema: Ewe Muhammad nieleze kuhusu Uislamu.Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie: “Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana Mola anaeabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja.Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Kusimamisha Sala.Kutoa zaka.Na kufunga mwezi wa Ramadhani.Na kuhiji kwenye Nyumba tukufu ikiwa mnaweza kuifikia.”Mtu yule akasema: umepatia. Tukamshangaa mtu yule anamuuliza kisha anamsadikisha.Kisha akasema mtu yule: Basi niambie kuhusu Imani. Mtume Akasema: Imani ni Kumuamini Mwenyezi Mungu.Na Malaika wake.Na vitabu vyake.Na Mitume wake.siku ya mwisho.Na kuamini makadirio yake, ya kheri au shari.” Mtu yule akasema: Umesema kweli.Kisha akasema: “Basi nielezee kuhusu Ihsani(wema/ufanisi)” Akasema Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake):ni Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa humuoni, basi Yeye anakuona.Akasema mtu yule: Basi nielezee kuhusu Kiyama).” Mtume Akasema: anaeulizwa si mjuzi zaidi kuliko muulizaji. Akasema mtu yule: Basi nielezee ishara zake, Mtume akasema: “ni mjakazi atakapomzaa bosi wake,Na kuwaona wasio na viatu, walio uchi, wachungaji wa kondoo wakishindana kujenga majumba ya kifahari.Msimulizi anasema: Kisha mtu huyo akaondoka, nikatulia muda kidogo, kisha Mtume akaniambia: Omar, umemjua ni nani muulizaji? Nikasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: Ni Malaika Jibril amekuja kuwafundisheni dini yenu.)

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

 “Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao”.

[Al-Baqarah: 177].

“Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako”.

[Al-Baqarah: 285].

“Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya mwisho, basi huyo amekwisha potelea mbali”.

[An-Nisa: 136].


 “Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo”.

[Al- Qamar: 49].

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti”.

[Al- Bayyinat: 5].


 “Enyi mlio amini! Mmefaradhishiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu”.

[Al-Baqarah: 183].

Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu”.

[Al Imran: 97]

Miradi ya Hadithi