عن أبي هُرَيرة رضي الله عنه، قال: خطَبَنا رسولُ الله ﷺ، فقال: «أيُّها الناسُ، قد فرَضَ اللهُ عليكم الحجَّ؛ فحُجُّوا»، فقال رجُلٌ: أكلَّ عامٍ يا رسولَ الله؟ فسكَتَ حتى قالها ثلاثًا، فقال رسول الله ﷺ: «لو قلتُ: نَعمْ، لوجَبتْ، ولَمَا استطعتم». ثم قال: «ذَروني ما تركتُكم؛ فإنما هلَك مَن كان قبلَكم بكثرة سؤالهم، واختلافهم على أنبيائهم، فإذا أمرتُكم بشيءٍ فأْتوا منه ما استطعتم، وإذا نَهيتكم عن شيء فدَعوه»


Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Amani iwe juu yake alituhutubia na kusema: “Enyi watu, Mwenyezi Mungu amekufaradhisheni Hija; nendeni mkahiji, Akasema mtu mmoja : Je ni kila mwaka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Alinyamaza hadi akasema mara tatu. Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie: “Lau ningesema: Ndio, ingeli kuwa ni wajibu, na msingeliweza. Kisha akasema: Niachieni katika yale ambayo sikukuambieni. Waliangamia walio kuwa kabla yenu kwa sababu ya wingi wa maswali  na kutofautiana kwao na Manabii wao .. Basi nikikuamrisheni kufanya jambo, basi lifanyeni kadiri muwezavyo, na nikikukatazeni, basi liacheni.” 

Muhtasari wa Maana

Mtume rehma na amani zimfikie aliwaambia maswahaba zake kwamba Hijja ni wajibu kwao, na mmoja wao akamuuliza: Je, ni wajibu kuhiji kila mwaka? Basi Mtume Rehema na Amani zimshukie akakaa kimya na hakujibu, na mtu huyo akarudia tena wala hanyamazi, hivyo akawaambia waridhike na yale aliyoyasema, na akawa hakuwatilia uzito katika nafsi zao. Kwa kuwa kujitilia uzito wenyewe kwa kuuliza; Ndio ilikuwa sababu ya kuangamia kwa mataifa yaliyopita.

Miradi ya Hadithi