عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ - رضي الله عنه - أَنَّ رَسُولَ اللهِ قَالَ: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَإِذَا طَلَعَتْ مِنْ مَغْرِبِهَا، آمَنَ النَّاسُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ، فَيَوْمَئِذٍ ﴿لَا يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا﴾ [الأنعام: 158]».

Kutoka kwa Abu Hurayrah-Mwenyezi Mungu amuwiye radhi - kwamba Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:

Kiyama hakitasimama mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.Litakapo chomoza kutoka magharibi watu wote wataamini kwa pamoja.Siku hiyo: “kuamini hakutomfaa mtu chochote, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake”. [Al-An’am: 158]

  1. Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) anafahamisha juu ya alama kubwa ya mwisho ya kiyama, ambayo ni kuchomoza kwa jua kutoka upande wa magharibi kwa njia isiyo ya kawaida; Katika Hadith sahihi, jua linapotua, huenda kusujudu chini ya Arshi -kiti cha enzi- Basi linaomba ruhusa, na linapewa ruhusa, na linakuwa karibu na kusujudu, lakini halitakubaliwa, na litaomba ruhusa, na halitaruhusiwa, bali litaambiwa: Rudi ulikotoka na uchomoze kutoka upande wa magharibi. [1]

  2. Jua linapochomoza kutoka magharibi, watu wote watamwamini Mwenyezi Mungu, na ni imani ya lazima ambayo hakuna khiyari. Ambapo yatakuwa yameshaonekana mambo yaliyo fichikana, na watu wote watakuwa na uhakika kwamba kiyama kimefika, hivyo wataamini kwa tamaa ya wokovu.

  3. Isipokuwa mlango wa toba utafungwa wakati huo, basi haikubaliwi toba kutoka kwa mwenye dhambi, wala Uislamu kutoka kwa kafiri; Kwani hiyo itakuwa ni  imani ya lazima iliyotokea baada ya kuona matukio makubwa, kwa hivyo hakuna faida ya imani hiyo, kwa kuwa imani hiyo ni kama ya wale waliofikiwa na kifo. Mwenyezi Mungu amesema:

    “Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia”.

    [Al Nisaa: 18]

    Na akasema Mtume Rehma na Amani zimshukie: “Mwenyezi Mungu anaikubali toba ya mja maadamu hayuko katika sakarati”[2] .pia hali hiyo ni kama Imani ya mtu ambaye ameteremshiwa adhabu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu Firauni:

    “Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana Mwenyezi Mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea (90) Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi”

    [Yunus: 90, 91].

Mafunzo

  1. Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameficha muda wa kusimama Kiyama ili mtu awe na bidii na utayari kwa ajili yake kila wakati, kwa kufanya hivyo utiifu wake utaongezeka na kupandishwa daraja lake, kama alivyoifanya Laylatul-Qadr kutokuwa wazi ili mja kujitahidi kuitafuta katika siku zote kumi. Haitakiwi kwa mtu kujua kiyama kitakuwa lini, lakini anapaswa kujitayarisha na kufanya mambo mengi ya kheri. Ndio maana mtu mmoja alipomuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni lini kiyama? Yeye, amani iwe juu yake, akasema: “umekiandalia nini?” [3].

  2. Lifanye kuwa kubwa jambo la kiyama katika nafsi yako, kwani jambo lake ni kubwa, na mpangilio wa dunia hubadilika wakati huo, jua litachomoza kutoka magharibi, basi dumu katika kuikumbuka na uiogope.

  3. Mwanadamu anatakikana kutubia kwa Mwenyezi Mungu haraka sana, kabla ya kufikiwa na mauti ghafla tu, au kwa jambo linalozuia kutubia. Amesema Bakr al-Muzni – Mwenyezi Mungu amrehemu –: “Hakuna siku ambayo Mwenyezi Mungu huileta duniani isipokuwa husema: Ewe mwana wa Adam, nifanye mimi kuwa ni fursa nzuri; Huenda isiwepo siku nyingine baada yangu, wala isiwepo usiku wowote isipokuwa huita kwa kusema: Mwana wa Adamu, nifanye mimi kuwa ni nafasi nzuri; Huenda usiwepo usiku mwingine baada yangu.” [4]

  4. Al-Bukhari, Mwenyezi Mungu amrehemu ni miongoni mwa walioisimulia Hadithi hii, na alikuwa miongoni mwa waliotumia vizuri fursa ya umri wake, na alikuwa akisema:

Pata faida ya muda wako kwa kuzidisha ibada = labda kifo chako kitakuwa cha ghafla.

Ni wangapi wamekufa bila ugonjwa = ghafla tu Nafsi zao zikatoka katika hali ya uzima

5.    Wengine wakasema:

Ionyeshe Nafsi yako uzito wa Siku ya Kiyama ewe mwenye kudanganyika, wakati mbingu zitakapokuwa na mgongano.

Wakati jua la mchana litakapo kunjwa na kushushwa = mpaka likawa juu ya vichwa vya waja.

Na nyota zitakapoanguka na kutawanyika = na kubadilika baada ya mwanga kuwa giza.

Na milima itakapong'olewa mizizi yake = utaiona inapepea kama mawingu

Marejeo

  1. Al-Bukhari (3199) na Muslim (159).
  2. Al-Tirmidhiy (3537) na Ibn Majah (4253).
  3. Al-Bukhari (7153) na Muslim (2639).
  4. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (2/391).


Miradi ya Hadithi