عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «خُلِقَتِ الْمَلَائِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ»
عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «خُلِقَتِ الْمَلَائِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ»
Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie“Malaika waliumbwa kutokana na Nuru,Majini wameumbwa kwa Moto.Adam aliumbwa kwa jinsi mlivyoelezwa”
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura (26) Na majini tuliwaumba kwa Moto”
[Al-Hijr: 26, 27].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
“Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo (12) Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti (13) Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji”
[Al- Mu-uminuuna: 12-14].
Amesema Mwenyezi Mungu
“Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo (14) Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto”
[Al-Rahman: 14, 15].
Na akasema pia:
“Moto huo Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa”
[Marufuku: 6]