عن النَّوَّاس بن سَمْعانَ رضي الله عنه قال: سألتُ رسولَ الله ﷺ عن البِرِّ والإثمِ، فَقالَ: «البِرُّ حُسْنُ الخُلُقِ، والإِثْمُ ما حاكَ في صَدْرِكَ، وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عليه النَّاسُ».

Kutoka kwa Al-Nawwas bin Samaan, Allah amuwiye radhi, amesema: 1- Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie kuhusu wema na dhambi. 2- Akasema: “Wema ni kuwa na tabia njema. 3- Na dhambi ni ile inayokutia wasiwasi kifuani mwako, na unachukia watu kuijua”

Muhtasari wa Maana

Al-Nawwas, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alimuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam juu ya wema na dhambi ni nini, akamwambia kuwa jambo linalo kusanya wema ni tabia njema, na dhambi ni kile unachokishuku, na hujatulizana kwayo, na unaogopa kwamba watu watajua kwamba unafanya hivyo

Miradi ya Hadithi