2 - KUSHUHUDIA KUWA HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ISPOKUWA ALLAH:

عَن مُعاذِ بنِ جبلٍ ‏‏رضى الله عنه قال:كنتُ رَدِيفَ النبيِّ ﷺ على حمارٍ، فقال: «يا معاذُ!، أتدري ما حقُّ اللهِ على العبادِ؟ وما حقُّ العبادِ على اللهِ؟» قلتُ: اللهُ ورسولُه أعلمُ. قال: «فإنَّ حقَّ الله على العبادِ أن يعبدوه ولا يُشركوا به شيئًا.وحقَّ العباد على الله أن لا يُعذِّب مَن لا يُشرك به شيئًا».قلتُ: يا رسول الله، أفلا أُبشِّر الناس؟ قال: «لا تُبَشِّرْهم فيتَّكلوا» متفق عليه.

Kutoka kwa Mua’dh ibn Jabal (r.a) amesema:

1. Nilikuwa nimepanda nyuma ya Mtume (s.a.w) katika mnyama. 

2. Akasema Mtume (s.a.w): “ewe Mua’dh! Je, wajuwa ni ipi haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake? na ni ipi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu”?  3.Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi juu ya hilo. 4.Akasema Mtume (s.a.w): “hakika haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake ni kumuabudu yeye peke yake wala wasimshirikishe na chochote 5. Na haki ya waja juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kutomuadhibu yeyote asiemshirikisha na chochote” 

6.Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je nisiwabashirie watu? Akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: “Hapana usiwape bishara hii, kwani watakuwa wavivu”

Msimulizi: jina lake anaitwa: Abu al- Abbas, Abdullah bin Abbas

Msimulizi: jina lake anaitwa: Abu al- Abbas, Abdullah bin Abbas bin Abdul Muttalib, al- Qurashi, al-Hashemi, al- Madani, alizaliwa katika watu wa Bani Hashim miaka mitatu kabla ya kuhama, na yeye ni mwanzuoni nguri katika ummah huu, na mtafsiri hodari wa Qur'an, binamu wa Mtume wa Allah,  rehma na Amani zimshukie, na alikuwa akiitwa: bahari, kwa sababu ya elimu yake kubwa, Mtume (rehema na amani za Allaah ziwe juu yake) alikumombea dua kwa kusema: "Ewe Allah, mfahamishe elimu ya dini 1 ", na yeye ni mmoja wa maswahaba walisimulia hadithi nyingi, alisemulia hadithi (1696) kutoka kwa Mtume (rehema na amani za Allaah zimshukie) aliingia katika uislamu akiwa kijana mdogo, na akalazimiana na Mtume (rehema na amani za Allaah zimshukie) baada ya vita ya ufunguzi   makkah, na alipokufuka macho mwishoni mwa maisha yake, na alifariki katika mji wa Taif mwaka (68 AH)  .

Miradi ya Hadithi