1- Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anawaelekeza waumini wajitahidi na kushindana kutenda mema kabla fitina kubwa haijaingia, itakuwa ni mfano wa usiku mweusi wenye kiza totoro, hakuna mwezi wala mwanga, haionekani haki wala batili. amesema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “hakika huu Umma wenu, salama yake iko mwanzoni, huko mwisho watapatwa matatizo na mambo ambayo mtaona kweli ni mabaya, inakuja fitina inafikia hatua wanaanza kutekana na kufanyana watumwa wao kwa wao, inakuja fitina, muumini anasema: hii inaniangamiza, hii inaniangamiza. Kisha inaondoka. Inakuja fitina, muumini anasema: hii sasa ndiyo inanimaliza”[1]. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameamrisha kujitahidi kufanya mema kabla fitina haijaingia na kuenea; kwa sababu katika kipindi cha fitina ibada inakuwa nzito sana, kwani nafisi inajishughulisha na fitina jambo ambalo linapelekea ibada kudhoofika, na ndio maana Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akasema: “Ibada katika kipindi cha fitina, ni sawa na kuhama kuja kwangu”[2] yaani mji wa Madina. Na akasema: “itafikia zama mtu atakae vumilia kuishika Dini yake, ni kama mtu aliye shika kaa la moto”[3]
2- Kisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akaeleza kwamba, fitina hizo zina uwezo mkubwa wa kumshambulia mtu, kiasi kwamba zinamtoa mwislam katika dini yake haraka sana, ni kama tu ni ndani ya mchana mmoja. kwa sababu nyoyo ni nyepesi kubadilika na kuiacha haki, zinapenda sana upotevu, zikikosa ndani yeke kinga, zinapata maradhi mabaya na kuziua”[4]. Kwa kuwa mitihani na matatizo ikikithiri kwenye nafsi inaziharibu kwa kuzizidia na kuzisababishia kuwa ngumu[5].
3. Kwa hali kama hiyo, mtu anaweza kuiuza dini yake kwa kitu kidogo katika Dunia, inaweza kuwa ni mali au cheo au vinginevyo katika mapambo haya ya Dunia yenye kuisha
MAFUNDISHO
1. Pupia kufanya mema, kama ibada, kusoma, kufundisha, kuoa, kuunganisha ndugu na mengineyo. Usiendekeze matarajio kwa kujichelewesha mpaka kesho au kesho kutwa, au kwa kusema, nikikuwa, au nikipata kitu fulani. Mitihani ambayo inamkwaza mtu kutekeleza dini yake na ibada zake inaweza ikateremka, pupia kwa juhudi kabla vikwazo havijashuka.
2. Mara nyingi mtu hafanyi ibada kwa sababu anataka afikie kiwango anacho kiwaza, nikama mtu anachelewesha kusambaza kitabu kwa kusubiri kila kitu kitimie, au anachelewesha kumapatia mke wake zawadi mpaka ikamilike, au hasomi Qur`an wala hasikilizwi mpaka ajiweze, ataendelea kuahirisha mpaka anabanwa na majukumu, au anakata tamaa au vinginevyo. Lau angelifanya anacho kiweza, angelipata wepesi kwa kiasi kikubwa.
3. Kuwa msitari wa mbele katika mambo mema ni ustadi, anajifunza mwanadamu kwa kukithirisha kuwa msitari wa mbele yeye mwenyewe, itakuwa ni kazi ngumu mwanzoni na ataichukia, kisha baada ya muda itakuwa nyepesi, inamvutia kuifanya kadri awezavyo. Jizoeshe kuwa mstari wa mbele kwa matendo mema, na uhesabu ni mara ngapi umekuwa mstari wa mbele kwa kutoa maneno mazuri, au sadaka au kusaidia mtu kwa tatizo lililo mpata bila matarajio, sawasawa ni ndugu au si ndugu.
4. Jikurubishe kwa Mwenyezi Mungu ukiwa na raha, atakukumbuka ukiwa na matatizo. kuwa msitari wa mbele kwa matendo mema pindi unapokuwa na wasaa, afya na unajitambua. Namuomba Mwenyezi Mungu akulinde na fitina.
5. Inatakiwa mwislaam akithirishe kumuomba Mwenyezi Mungu amjaalie ashikamane na dini yake, na asimpatie mitihani; Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) mara nyingi alikuwa akisema: “Eh Mwenye kubadisha nyoyo, ujalie moyo wangu ushikamane na dini yako”[6].
6. Mwanadamu anapokuwa amezama katika fitina, huenda asitambue kwamba anauza dini yake, anaweza kupuuzia miamala ya kifedha, au ardhi, kwa kuzidishiwa ambacho si haki yake, au huenda akasengenya, au akaacha kusengenya ili kumridhisha tajiri yake. Jifuatilie mwenyewe na ujitathmini, na wala jicho lako lisitizame panapo dhuru Imani yako, Dini ndio kitu cha thamani zaidi.
7.Amesema mshairi:
Kuwa msitari wa mbele madamu umri bado upo***uadilifu wako unakubalika na ulicho kitoa ni cha thamani .
Jitahidi, pupia na utumie ujana***kwani ni muda unaoweza kuutumia ukafaidika.
Fanya haraka, kwani kifo kiko nyuma yako kinakuja kwa kasi***haiwezekani hata kidogo kukikwepa au kukishinda.
Marejeo
- Muslim (1844), kutoka kwa Abdullah bin Amr bin Al-Aas, Mungu awe radhi nao
- .Muslim (2948),kutoka kwa Ma’qil ibn Yasar
- Al-Tirmidhiy (2260), kutoka kwa Anasa
- l'iifsah an ma`ani alsahahi" cha Ibn Hubayrah (8/163).
- “Al-Mufhim lamaa 'ushakil min talkhis kitab Muslim” cha Al-Qurtubi (1/326)
- . Ahmad (12107), al-Tirmidhiy (2140), na Ibn Majah (3834).