136 - KUACHA HADITHI ZA NAFSI BILA MATENDO

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَتَكَلَّمْ»

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ambaye amesema: “Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wangu kwa yale waliyojisemea ndani ya Nafsi maadamu haukufanya wala kusema.” 

Muhtasari wa Maana

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, anatuambia kuwa Mwenyezi Mungu, Utukufu ni wake, ameondosha kwa neema yake, yote yanayopita katika Nafsi zetu, miongoni mwa matamanio, matakwa, fikra na yanayojiri moyoni. Hatutawajibishwa kwa jambo ambalo hatukusema au kufanya kwa viungo vyetu.

Miradi ya Hadithi