21 - FADHILA ZA KARNE YA KWANZA KATIKA WAJA WEMA

عَنْ عِمْرَانَ بْنَ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «خَيْرُ أُمَّتِي قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ - قَالَ عِمْرَانُ: فَلاَ أَدْرِي، أَذَكَرَ بَعْدَ قَرْنِهِ قَرْنَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا؟ - ثُمَّ إِنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يَفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمُ السِّمَنُ».

Kutoka kwa Imran bin Huswaein, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie.““Umma Bora ni karne yangu.Kisha wale wanaowafuataKisha wale wanaowafuataImran akasema: Sijui alitaja karne mbili au tatu baada ya kizazi chake? -Kisha kutakuwa na watu baada yenu ambao watashuhudia lakini hawatauawa kishahidi.Wanafanya khiyana na hawaaminiki.Wanaweka nadhiri lakini hawazitimizi.Unene na vitambi vitadhihiri kwao

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anafahamisha kuwa watu bora zaidi ni maswahaba wake wanaoishi zama zake, kisha wanaowafuata na wafuasi wao baada yao. Kisha Mtume, amani iwe juu yake, akaeleza kuhusu upotovu wa wale walio baada ya karne hizo bora, na akataja kwamba wanadharau ushahidi, wanasaliti amana, na hawatimizi yale wanayojiwajibishia, na watakua na athari ya kupenda dunia na starehe yake.

Miradi ya Hadithi