عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ يَقُولُ: «ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ: مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا»

Kutoka kwa al-Abbas ibn Abd al-Muttalib

(Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) akisema: 1.“Ameipata ladha ya imani. 2. Aliyemridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi  3. Na Uislamu kuwa Dini aliyoichagua. 4. Na Muhammad kuwa ndio Mtume wa haki”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Na miongoni mwao wapo wanao kusengenya katika kugawa sadaka. Wanapo pewa wao huridhika. Na wasipopewa hukasirika (58) Na Kama wao wangeli ridhia kile alicho wapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila zake - na pia Mtume wake; hakika sisi tunataka radhi za Mwenyezi Mungu”.

[At-Tawbah: 58-59].

Amesema mtukufu aliye tukuka: 

“Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo jidhulumu wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu (64) La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayo toa, na wanyenykee kabisa”.

[An-Nisa: 64, 65د

Miradi ya Hadithi