عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ يَقُولُ: «ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ: مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا»

Kutoka kwa al-Abbas ibn Abd al-Muttalib

(Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) akisema: 1.“Ameipata ladha ya imani. 2. Aliyemridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi  3. Na Uislamu kuwa Dini aliyoichagua. 4. Na Muhammad kuwa ndio Mtume wa haki”

Muhtasari wa Maana

Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema kwamba Imani ina matunda matamu sana ambayo hawezi kuyaonja isipokuwa mwenye moyo uliojaa Imani. Kwa kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi, na akafanya Uislamu kuwa ndio Dini aliyoiridhia na kuiamini, na akanyenyekea kwa Mtume wake Muhammad (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake), na kukiri Utume wake na wajibu wa kumuamini.

Miradi ya Hadithi