150 - UTUKUFU WA KUWA NA MATARAJIO MAZURI KWA ALLAH

عَنْ أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضي الله عنه، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ يَقُولُ: قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: «يا بْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي، غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي. يا بْنَ آدَمَ، لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي، غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي.يا بْنَ آدَمَ، إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأرضِ خَطَايَا، ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا، لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً

1- Kutoka kwa Anas bin malik radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:

Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie akisema: Mwenyezi Mungu aliyetukuka amesema: “Ewe mwana wa Adam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe kwa yale yaliyokuwa ndani yako, wala sijali. 2- Ewe Mwana Aadam hata kama dhambi zako zikifika kwenye mawingu ya mbingu, kisha ukaniomba msamaha, nitakusamehe na sitojali.  3- Ewe Mwana Aadam, kama utanijia na madhambi makubwa kama ardhi, kisha ukakutana Nami hukunishirikisha na chochote, nitakupatia msamaha sawa na ukubwa wa madhambi” 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mtukufu anasema:

“Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo jidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu”.

[An-Nisa: 64]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” .

[Al-Furqan: 70]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” .

[Al-Zumar: 53]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe” .

[Nuhu: 10]

Miradi ya Hadithi