عَنْ طَلْحَةَ بْنِ عُبَيْدِ اللهِ رضي الله عنه قَالَ:جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللهِ مِنْ أَهْلِ نَجْدٍ، ثَائِرُ الرَّأْسِ، يُسْمَعُ دَوِيُّ صَوْتِهِ، وَلَا يُفْقَهُ مَا يَقُولُ، حتَّى دَنَا، فَإِذَا هُوَ يَسْأَلُ عَنِ الإِسْلامِ،فَقَالَ رَسُولُ اللهِ : «خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي اليوْمِ وَاللَّيْلَةِ»، فَقَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ رَسُولُ اللهِ : «وَصِيَامُ رَمَضَانَ»، قَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهُ؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ: وَذَكَرَ لَهُ رَسُولُ اللهِ الزَّكَاةَ، قَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ: فَأَدْبَرَ الرَّجُلُ وَهُوَ يَقُولُ: وَاللهِ، لَا أَزِيدُ عَلَى هَذَا وَلا أَنْقُصُ. قَالَ رَسُولُ اللهِ : «أَفْلَحَ إِنْ صَدَقَ». وفي رِوايةٍ: «دَخَلَ الجَنَّةَ إِنْ صَدَقَ»

Kutoka kwa Talha bin Ubaydillah Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yakeamesema:

  1- Alikuja mtu mmoja katika watu wa Najd kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), Sauti yake inasikika, lakini haeleweki anachosema, mpaka akakaribia, kumbe anauliza kuhusu Uislamu  2- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Swala tano kwa mchana na usiku", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? Akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”.  

3- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Na Saumu ya Ramadhani", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”.  

4- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), akamtajia Zaka, akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: Hapana, isipokuwa ukijitolea.  

5- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Basi yule mtu akageuka na kusema: Wallahi siwezi kuongeza wala kupunguza katika haya.  

6- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Atafaulu ikiwa ni mkweli." Na katika riwaya nyingine: “Ataingia Peponi ikiwa anasema kweli. 

1.     Mmoja wa Mabedui aliingia  akitokea eneo la  Najd - Ni uwanda unaoenea kutoka Hijaz upande wa mashariki hadi Al Yamaamah upande wa magharibi, sasa inajumuisha Riyadh, Qassim na Aflaaj [1] – kwa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake),  akiwa amekaa na maswahaba zake, na huyo bedui alikuwa na nywele zilizo chakaa, asiyejali muonekano wake, akiwa anaita kwa mbali na kusema kwa sauti kubwa, sauti yake inasikika, na anachosema hakieleweki, Alipokaribia mkusanyiko ule, walielewa maneno yake, kumbe alikuwa anauliza kuhusu sheria za Uislamu[2]


2.     Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake),  akamuelezea faradhi ya swala, kwamba ni nguzo ya pili ya Uislamu baada ya shahidi mbili, na kuna Swalah tano juu yake mchana na usiku, nazo ni Fajr, Dhuhr, Asr, Maghrib na Isha. Bedui akamuuliza: Je, ni wajibu kwangu kufanya jambo jengine iwapo nitazitekeleza swalah hizi na kutekeleza nguzo, wajibaat na kwa kusali kama ipasavyo? Nabii akajibu (Rehema na amani ziwe juu yake), si wajibu kwake isipokuwa Swalah hizo, ila kwa kujitolea. 

Kujitolea: Ni kwamba mja ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa njia ya ibada ambayo si lazima kwake, kwa kutamani kupanda daraja Siku ya Kiyama, haya ni matendo yaliyohimizwa yafanywe, mwenye kuyafanya analipwa, na asiyeyafanya hataadhibiwa[3]


3.Kisha Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) akataja swaumu ambayo ni nguzo ya nne ya Uislamu, na maana yake ni; kujiepusha na vyakula, vinywaji, na mambo mengine yote yanayofungua saumu, kuanzia mapambazuko ya alfajiri ya kweli hadi kuzama kwa jua, kwa nia ya kutafuta malipo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu[4]. Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), akamwambia kwamba ni lazima afunge mwezi wa Ramadhani, Bedui akamuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake): Je, inanilazimu kufunga tofauti na mwezi huu? Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) pia akamjibu kuwa si wajibu kufunga isipokuwa Ramadhani, ila kufunga kwa hiari katika siku zingine ambazo si lazima kufanga. 

4.Kisha Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake)  akamueleza Zaka, ambayo ni nguzo ya tatu ya Uislamu baada ya shahada mbili na swala, akamwambia kuwa ni wajibu, na akambainishia hukumu zake. 

Zaka: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutoa sehemu ambayo ni wajibu kisheria juu ya mali maalum kwa ajili ya watu au kazi maalumu[5]. Bali, iliitwa zakat kwa sababu inaitakasa nafsi na kuisafisha kutokana na dhambi.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo”

[At-Tawbah: 103]. 

Basi yule mtu akamuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake): Je, ni lazima nitoe pesa zangu zaidi ya ile Zaka iliyofaradhishwa? Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake):  akasema: Hapana, isipokuwa kujitolea na kutoa pesa zako kwa njia za kusaidia katika mambo ya kheri. 


5.Kisha yule mtu akaondoka na kusema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, siwezi kuongeza katika haya wala kupunguza.” yaani, atatekeleza vile inavyopaswa, bila kuongeza au kupunguza, Kama unavyomwambia aliyekupangia kazi: Sitaongeza wala sitapunguza. 

makusudio ya mtu huyo si kwamba atakomea kwenye amri hizo na kuacha mengine yote ambayo Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) hakutaja, kama vile kuinamisha macho, kuzilinda tupu, kutekeleza amana, kusema kweli, na mengineyo; kwa sababu huo ni uovu haifai kwake kuusema, na Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) hawezi kumkubalia jambo kama hilo, bali alimuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake)  juu ya matendo na faradhi zitakazomfikisha Peponi, ndio maana hakumwambia juu ya kuepuka makatazo na mengineyo. 

Kama ilivyo kwa mwenye kushikamana na aliyoamrishwa kwa kiwango hiki, inapomjia amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa Mtume wake, basi huikimbilia kuitekeleza, na wala haiachi, iwe ni faradhi au Sunnah[6]

6.Basi Mtume, (Rehema na amani ziwe juu yake) akasema kwamba, huyo mtu akitimiza hayo na akawa mkweli, basi amefaulu na ameshinda kwa kupata kila lililo la kheri. 

Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake)  hakuzitaja shahada mbili; kwa sababu alijua kwamba anazijua, au kwa sababu alikuja kumuuliza kuhusu sheria za kivitendo za Uislamu, vile vile hakumbainishia Hija kwa sababu ilikuwa bado haijawajibishwa, au labda haikuwa wajibu kwake, au aliitaja na msimuliaji akaifupisha hadith[7]


MAFUNDISHO 


1.Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), alivumilia ukali wa Bedui huyo na kumpandishia sauti, katika hili yapo mafunzo kwa mlinganiaji, mwalimu na mlezi kwamba inatakiwa awe na subira na kuvumilia taabu za Da’wa; Anaweza kukutana na makosa au maudhi; Ni lazima awe na uvumilivu, na kufuata mfano wa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake). 

2.Mlinganiaji, msimamizi, msomi na mlezi lazima wazingatie tofauti za kiakili baina ya watu,  wasitumie njia moja kuishi na watu wote, Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), hakumkosoa  bedui kwa kunyanyua sauti yake, wala kumlaumu kwa hilo. 


3.Mtu huyo alikuwa amependa sana kumuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), juu ya yale ambayo yatamnufaisha bila ya kuwa na haya, Kila alipomuamuru kufanya jambo fulani, alisema: “Je, ni lazima nifanye jambo lingine?”. Mtu anapaswa kuwa na bidii ya kutafuta elimu, haya au kiburi haipaswi kumzuia kuuliza. 


5.Swalah za Sunna ni nyingi, za muhimu na zenye daraja ya juu zaidi ni Sunna zilizosisitizwa, zinazokuwa baada ya Swalah za faradhi, nazo ni rakaa mbili kabla ya Alfajiri, nne kabla ya Adhuhuri, mbili baada yake, mbili baada ya Almagharib, na mbili baada ya Al ishaa;

Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) amesema:

“Mwenye kuswali rakaa kumi na mbili mchana na usiku, atajengewa nyumba Peponi.[8]”

Ikiwa ni pamoja na Swala ya Duha, qiyaam al-layl (Swalah za usiku), Swala ya Witr, na Swala zingine za  Sunna ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema ndani ya Hadithi tukufu:

“Haachi Mja wangu kuendelea kujikurubisha kwangu kwa Sunna mpaka nampenda, basi nikimpenda, mimi ndiyo nakuwa sikio lake ambalo hutumia kusikia, na jicho lake ambalo hutumia kuona, na mkono wake ambao hutumia kushika, na mguu wake ambao hutumia kutembea, na akiniomba, nitampa, na akiniomba kinga, nitamkinga.[9]” 

6.Kujitolea kufunga ni mojawapo ya Sunna bora, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuandalia mwenye kujitolea kufunga malipo makubwa; Kufunga siku ya Arafah kunafuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka ujao[10]. Funga ya A’shuraa inafuta madhambi ya mwaka uliopita[11]. Anayefunga siku sita za Shawwal, baada ya Ramadhani ni sawa na kufunga mwaka mzima[12]


7.Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) ameitaja Zaka kwa sababu ni dalili ya imani ya mtu. Ni Muumini pekee ndiye anayetoa Zaka kwa ridhaa yake; Sababu ni kwamba nafsi inapenda mali na inafanya ubakhili kuzitoa, ikiwa itaruhusu kutolewa kwa ajili ya  Mwenyezi Mungu Mtukufu, hii inaonyesha ukweli wa imani yake kwa  ahadi na maonyo ya Mwenyezi Mungu. Mja hana budi kupima imani yake kwa kutoa Zaka na sadaka na kujizoesha kufanya hivyo, kwasababu yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu ni bora na yanadumu. 

8.Akasema Bedui: “Wallahi mimi siongezi juu ya haya wala sipunguzi”. Hii ni alipojua kwamba kutekeleza faradhi inatosha kuingia Peponi. Ni lazima mtu awe thabiti na mwenye bidii katika kila jema analofanya na kutarajia malipo yake, asirudi nyuma wala kukata tamaa baada ya kuanza, iwe katika matendo ya Akhera au ya Dunia. Mwanafunzi hapaswi kuwa mvivu katika kusoma masomo yake, na askari asichoke kulinda mpaka wake, na mkono wa ufanisi usikose kwa mfanyakazi na mtengenezaji wa vifaa mabalimbali hadi amalize kazi yake. 


9.kauli ya Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), baada ya maneno ya mtu huyo, ni ushahidi kwamba hii sio tu kwake, bali ni kwa kila Muislamu mwenye kutekeleza mambo ya faradhi ipasavyo, na kujiepusha na yaliyo haramishwa, hayo yanatosha kuwa sababu ya kusalimika na Moto wa Jahannam na kuingia Peponi. Ieleweke kwamba, Pepo ina daraja. Daraja la juu na bora zaidi, ni mja kuwa katika kundi la manabii, mitume, wakweli, mashahidi na watu wema. Hapana shaka kwamba daraja hii haipatikani kwa kutekeleza faradhi tu, kila mtu na ibada zake! Na kila mwanadamu na yale ambayo nafsi yake inayatamani huko akhera! 

10.Katika Hadithi, Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), alizingatia hali ya anaye linganiwa na muulizaji; Ndiyo maana hakumbainishia zaidi faradhi na nguzo ambazo zikikosa Uislamu wa yeyote huwezi kuwa sahihi. Mlinganiaji, mwanachuoni, na msomi, lazima awe mwerevu, amjibu muulizaji vizuri, na alinganie kwa namna inayoendana na hali mtu. 


11.Mshairi amesema: 

Kuinua mwito wa Swala juu ya minara = katika alfajiri ya asubuhi na usiku utulivu 

wito unaoleta uhai kwa ulimwenguni = na wakazi wake, vijiji na miji 

Na mwito kutoka mbinguni kwenda Ardhini = juu na ndani yake 

Na kukutana baina ya Malaika na = Imani na Waumini bila ya idhini 

Na kuondoka kwenye kufaulu, kheri =, haki, uwongofu, na wema. 

Mshairi mwingine amesema; 

Ewe mtoa sadaka mali ya Mwenyezi Mungu = katika njia za kheri, mali haipungui. 

Ni kiasi gani Mwenyezi Mungu amezidisha mali kwa mmiliki wake kuzitoa = Ukarimu ni kwa hukumu ya  Mwenyezi Mungu ni kupata radhi zake. 

Ubahili hupelekea ugonjwa ambao hauna tiba = Mali ya bahili kesho itakuwa urithi kwa wanaoteseka.  Sadaka ni furaha kwa wale wasio na uwezo = Watu wa ukarimu ukiwahitaji wanajitokeza. 


Marejeo

  1. Tazama:  "'Atlas Alhadith Alnabawi" cha Shawqi Abu Khalil (uk. 365)
  2. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (1/106)
  3. .Tazama: “Mughni Al-Muhtaaj” cha Al-Khatib Al-Sherbini (2/182)
  4. .Tazama: "Al-Sharh al-Mumti' ya  Zad al-Mustaqni'" cha Ibn Uthaymiyn (3/5)
  5. .“Al-Sharh al-Mumti’ kwenye Zad al-Mustaqni’” cha Ibn Uthaymiyn (6/13)
  6. .Sherh ya Sahih Al-Bukhari cha Ibn Battal (1/104-105)
  7. .Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (1/ 107)
  8. .Imepokewa na Muslim (728)
  9. .Imepokewa na Al-Bukhari (6502)
  10. .Imepokewa na Muslim (1162)
  11. .Imepokewa na Muslim (1162). 
  12. (Imepokewa na Muslim (1164


Miradi ya Hadithi