33 - KUKUSANYA KATI YA MATENDO NA KUAMINI MAKADIRIO

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «الْمُؤْمِنُ الْقَوِيُّ خَيْرٌ وَأَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنَ الْمُؤْمِنِ الضَّعِيفِ،وَفِي كُلٍّ خَيْرٌ.احْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ،وَاسْتَعِنْ بِاللهِ وَلَا تَعْجِزْ، وَإِنْ أَصَابَكَ شَيْءٌ، فَلَا تَقُلْ: لَوْ أَنِّي فَعَلْتُ كَانَ كَذَا وَكَذَا، وَلَكِنْ قُلْ: قَدَرُ اللهِ وَمَا شَاءَ فَعَلَ؛ فَإِنَّ (لَوْ) تَفْتَحُ عَمَلَ الشَّيْطَانِ» رواه مسلم

1.Kutoka wa Abuu Hurairah, amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake):  “Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, 2..Na wote wana kheri 3.Pupia jambo lenye kukunufaisha, 4.Na umuombe Mwenyezi Mungu msaada, 5.Jambo lolote likikusibu, usiseme: lau ningefanya hivi na hivi, 6.Badala yake sema: Ni mipango ni ya Mwenyezi Mungu, anafanya atakalo 7.Kwa sababu (lau) inafungua kazi ya shetani”



Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

 " Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua.”

[Al-Anfal: 60]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

95. " Hawawi sawa Waumini wanao kaa tu wala hawana dharura, na wale wanao pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewatukuza cheo wale wanao pigana kwa mali yao na nafsi zao kuliko wale wanao kaa tu. Ingawa Mwenyezi Mungu amewaahidi wote mashukio mema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhili wanao pigana kwa ujira mkubwa kuliko wanao kaa tu" .

[An-Nisa: 95]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

 " Na tendeni mema, ili mfanikiwe ".

[Hajj: 77]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

 "Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaad"a.

 [Al-Fatihah: 5]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

"Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanao subiri. "

[Al Imran: 146].

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

" Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe ". 

[Al Imran: 154]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

22. "Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 23. Ili msihuzunike kwa kilicho kupoteeni, wala msijitape kwa alicho kupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna akajifakhirisha". 

[Al-Hadid: 22, 23].

Miradi ya Hadithi