1. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anaeleza kwamba muumini mwenye nguvu anapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko Muumini dhaifu. Makusudio ya nguvu, inamaanisha nguvu ya kiimani na yote yenye kufanikisha uwepo wa Imani, kama nguvu ya nafsi, nguvu ya mwili, nguvu ya elimu na mfano wa hayo. Hivyo vikikutana, vinasaidia kufanya ibada, majukumu muhimu katika maisha, kuipambania dini na kufanya mambo yenye kukunufaisha wewe na jamii.
Amesema Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake):
“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua" . ”
. Nguvu hizi zinamfanya awe mvumilivu katika kufanya ibada na kuwa mbali na Maasi, eidha zinamuhimiza kuamrisha mema na kukataza mabaya, pia kumfanya astahamili maudhi ya watu na matatizo ya Dunia[1]
2.Kumtanguliza mwenye nguvu haimanishi kwamba dhaifu hana kheri yoyote, bali yeye pia ana kheri japo kiasi kikubwa kimempita. Usulubu wa maneno haya ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) unajulikana katika Lugha ya kiarabu kwa jina la (usluubul ihtiraas), yaani; usulub wa kuchukua tahadhari ya umakini katika mazungumzo.
3.Baada ya kubainisha kwamba muumini mwenye nguvu ni bora, akabainisha anapo takiwa kuelekeza nguvu zake, na haya ni miongoni mwa maneno machache yenye maana pana, kwa sababu yamemuelekeza ajitahidi katika kila lenye kumletea manufaa ya haraka au badaye, na akasisitiza alifanye na aache mambo ya kipuuzi
4.Muislam anapo pupia kufanya mambo yenye kumnufaisha katika Dini na Dunia yake, inatakiwa amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu msaada kwa kumtegemea katika kupata anacho tarajia, eidha asizembee wala kudhoofika na kushindwa kufikia malengo yake kwa kusingizia Qadar, yaani mipango ya Mwenyezi Mungu, udhaifu au vinginevyo bila kufanya juhudi, katika hali hiyo atalaumiwa kwa kupuuza na kupoteza malengo yake.
5.Muumini akipata kinyume na alicho kuwa anatarajia, asijute kwa juhudi na jitihada zake, na wala asiseme: “lau ningelifanya hivi na hivi, ingelikuwa hivi” kwa hasira na kuchukia mipango ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kwa kudhania kwamba mambo yangelibadilika lau angelibadilisha aliyo yafanya. Hakika mambo yote yanaenda kwa mipango aliyo iandika na Mwenyezi Mungu kabla ya kuumba mbingu na Ardhi, jukumu la mwanadamu ni kufanya sababu za kufikia anacho kihitaji, na matokeo anamkabidhi Mwenyezi Mungu.
6.Inatakiwa aseme: “mipango ni ya Mwenyezi Mungu, anafanya atakalo”[2]. Yaani awahi kusalimisha matokeo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na aseme: hii ni mipango ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na jambo hili limetokea kwa mipango yake aliyo andika itusibu, haliwezi kutokea lolote ila analolitaka.
Haimanishi kwamba asingizie Qadar yaani mipango ya Mwenyezi Mungu katika maasi na makosa, aseme: nimefanya maasi kwa Qadar ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi aliwakemea washirikina walio simamia hoja hiyo batili juu ya ushirikina wao,
amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“. Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivyo hivyo walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu ". .”
7.Mtume Mtukufu amezuia jambo hilo kwa sababu linafungua mlango wa shetani, zinaanza wasisi za kukanusha Qadar, yaani mipango ya Mwenyezi Mungu pale unapo chukia, kujilaumu na kushutumu kwamba haifai. Unabaki katika maisha ya huzuni, jambo ambalo linakufanya uwe dhaifu, upoteze muda na fursa nyingine. Na wala haimanishi kwamba neno (lau) ni haramu moja kwa moja, linakuwa haramu likitumika katika mazigira ya hasira na kulaumu na mfano wa hayo. Ama mwanadamu wakilitamka ili kubainisha kosa au hukumu ya kisheria au kuzungumzia mambo yajayo, inaruhusiwa, amesema Nabii Luut
“. Akasema: Laiti ningeli kuwa na nguvu kwenu, au nategemea kwenye nguzo yenye nguvu! ,”
Na amesema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “lau nisingeliogopea kuwawekea uzito umma wangu, ningeliwaamrisha kuswaki kila wanapotaka kusali”[3]. Na Abuu bakar swiddiiq (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake) amesema akiwa ndani ya pango na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “lau mmoja wao angelitizama chini ya mguu wake angelituona”[4]
MAFUNDISHO
- Nafsi iliyo salimika, inapenda kuwa bora katika mambo ya kheri, ushindani huu unapelekea kujituma ili kupata nafasi iliyo bora. Wahamasishe ulio nao, kama vile wanao au wanafunzi au wanao jitahidi kufanya mambo kikamilifu, wasaidie kwa kuwapatia maelekezo na msaada .
- Nguvu ni sababu ya kufikia malengo, jizoeshe kuwa mvumilivu na kufanya juhudi ya kupata nguvu za kukupelekea kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Sala, Zaka, Funga, Hija, Jihadi, yaani kuipambania Dini, kuamrisha mema na kuzuia mabaya, kuwafanyia wema wazazi, kuwaunganisha ndugu na mengineyo yanayo takiwa yafanywe au yaachwe, yote yanahitaji nguvu ya mwili, nafsi, elimu, na vinginevyo. Unapo kuwa na nguvu za kufanya jambo la kheri, mshukuru Mwenyezi Mungu, na unapo kosa, basi likabidhi kwake.
3. Ukimuona aliye jikatia tamaa, kwa sababu anajiona kuwa ni dhaifu katika elimu au biashara au nguvu ya kimwili au lolote, mpe moyo kwa sababu jitihada zake ni katika kheri.
4. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amekusanya katika kauli yake: “Pupia jambo lenye kukunufaisha, na umeombe Mwenyezi Mungu msaada” misingi miwili, nayo ni; kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa na imani naye, na kufanya sababu za kufikia unacho kilenga, ili kuendana na kauli ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:
“Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. ”
,”. Hivyo basi inampasa Mwanafunzi ajitahidi katika masomo yake, Na mwenye mradi autekeleze Kwa ufanisi Na ajitahidi kuhakikisha anafaulu, na mwalimu atoe elimu yake kwa ufanisi. Wote hao wamuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu msaada katika kukamilisha malengo yao na awajalie kufanikiwa kwa wanalo lifanya.
5. Kushindwa ni janga lenye kuwakosesha wengi mafanikio yao. Utakuta wanapenda kufanya jambo la kheri, kisha wanalikuza katika nyoyo zao, wanapatwa na udhaifu na kuliacha, mara nyingine wanaanza kulifanya, kisha azima yao inarudi nyuma na kushindwa kulikamilisha, wanachoka na kuacha. Inatakiwa mwanadamu ajikaze na achangamke, wala asizembee.
6. Haifai kwa mwanadamu kutamka matamshi yanayo mkasilisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama kuitukana Qadar yaani mipango ya Mwenyezi Mungu, mfano kusema: kwa nini iwe ni mimi?! Kwa nini iwe ni fulani?!, au kusema (lau) kwa hasira na kupinga Qadar.
7. Inatakiwa mwanadamu apupie lenye kumnufaisha katika mambo yake ya kidini na ki dunia, akiwa anatekeleza wajibu wake katika Dini, asisahau Dunia yake na anao wasimamia. Bali apupie kusoma elimu ya kiDunia, kuchuma riziki ya halali, kuhifadhi afya na mengineyo
8. Ukikosea, muombe Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha, na ukipatwa na msiba au tatizo sema “Innaa lillaahi wainnaa ilaihi raaji’uun” sote ni wa Mwenyezi Mungu na sote tutarejea kwake, na useme “Qadarullaah, wamaa shaa-a fa’la” Ni mipango ni ya Mwenyezi Mungu, anafanya atakalo. Acha kujilaumu sana, kuwaza na kutamani kwamba ingelikwa kinyume na ilivyo pangwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, hilo linapelekea kuchukia Qadar na huzuni iliyo pitiliza, na yaliyo pangwa na Mwenyezi Mungu haiwezekani kuyabadilisha. Zingatia mustakbali wako na angalia linalo wezekana kufanyika, umuombe Mwenyezi Mungu msaada.
9. Amesema mshairi:
Mwanadamu atamuomba nani msaada zaidi ya Mola wake***na ni nani atakuwa ni msaada kwa kijana kipindi cha matatizo?
Na ni nani Mfalme wa ulimwengu na walimwengu***na ni nani mwenye kuondoa matatizo akiwa mbali au karibu?
Na ni nani mwenye kuepusha misiba na matatizo pindi yanapo teremka***hayo yote ni matendo yako eh Mola wangu?.
Marejeo
- Tazama: "Sharh al-Nawawi katika kitabu cha Muslim" (16/215), "Mirqat al-Maftahat Sharh Miskat al-Masbah" cha Ali al-Qari (8/3318), "Al-Shabab Wafez al-Awqat" kutoka katika darsa za Ibn Baz
- .Daliilu Al-Falihin” (1/243), na ikasemekana kuwa inajuzu kukaza daali, tazama: “Mirqat al-Maftahat Sharh Mishkat al-Masbah” cha Ali al-Qari (8/ 3318)
- .Al-Bukhari (7240)
- .Al-Bukhari (3653) na Muslim (2381).