عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله ﷺ فقال: يا رسول الله، من أحق الناس بحسن صحابتي؟ قال: (أمُّك) قال: ثم من؟ قال: (أمك)، قال: ثم من؟ قال: (أمك)، قال: ثم من؟ قال: (أبوك)، وفي رواية قال: (أمك، ثم أمك، ثم أمك، ثم أباك، ثم أدناك أدناك)



Kwa kutoka kwa Abu Huraira, Allah amuwiye radhi, amesema:

1. Alikuja mtu kwa Mtume rehma na amani zimshukie na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani katika watu anastahiki zaidi usuhuba wangu? 2. Akasema Mtume: (Mama yako) Akasema: Kisha nani? Akasema: (Mama yako), akasema: Kisha nani? Akasema: (mama yako) 3. Akasema: Kisha nani? Akasema Mtume: (Baba yako), na katika riwaya akasema: (Mama yako, kisha mama yako, kisha mama yako, kisha baba yako, 4. Kisha anafuatia aliye karibu yako”

Muhtasari wa Maana

Swahaba mmoja, alimuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu watu wanaostahiki zaidi kuhurumiwa na kukirimiwa, na Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, akamjibu kuwa mama ndiye mtu pekee anayestahiki zaidi hayo, na akarudia mara kwa mara, kisha mara ya nne akamsifu baba, kisha jamaa wa karibu zaidi kisha wa karibu zaidi.

Miradi ya Hadithi