21 - FADHILA ZA KARNE YA KWANZA KATIKA WAJA WEMA

عَنْ عِمْرَانَ بْنَ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «خَيْرُ أُمَّتِي قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ - قَالَ عِمْرَانُ: فَلاَ أَدْرِي، أَذَكَرَ بَعْدَ قَرْنِهِ قَرْنَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا؟ - ثُمَّ إِنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يَفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمُ السِّمَنُ».

Kutoka kwa Imran bin Huswaein, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie.““Umma Bora ni karne yangu.Kisha wale wanaowafuataKisha wale wanaowafuataImran akasema: Sijui alitaja karne mbili au tatu baada ya kizazi chake? -Kisha kutakuwa na watu baada yenu ambao watashuhudia lakini hawatauawa kishahidi.Wanafanya khiyana na hawaaminiki.Wanaweka nadhiri lakini hawazitimizi.Unene na vitambi vitadhihiri kwao

Imran bin Husayn bin Obaid Al-Khuza’i

Yeye ni: Imran bin Husayn bin Obaid Al-Khuza’i, Abu Nujaid, alisilimu mwaka wa 7 Hijiriya, na alikuwa kiongozi alieshikilia bendera ya ukoo wa Khuza’ah siku ya ufunguzi wa makkah. Umar ibn al-Khattab Mwenyezi Mungu awe radhi naye alimtuma Basra huko Iraq, ili kuwafundisha watu dini yao, naye alikubali agizo hilo, na hakushuhudia fitna, alifariki mwaka wa 53 Hijiria [1].

Marejeo

  1. Rejea tafsiri yake katika: “Maarifaat al-Sahaba cha Abu Naim” (1/38), “Asad al Ghaba cha Ibn al-Atheer” (4/137), “Al-Isbah cha Ibn Hajar” (4/484)

Miradi ya Hadithi