عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ قَالَ: «لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لأَخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ»

Kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume rehma na amani zimshukie amesema:

“Hatokuwa na imani yeyote miongoni mwenu mpaka ampendelee nduguye kile anachojipendelea” 



Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mtukufu aliyetukuka: “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao”.

[Al-Fath: 29]

Na amesema aliye tukuka : “Hakika Waumini ni ndugu” .

[Al-Hujraat: 10]

Pia Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa na choyo ya nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa” .

[Al-Hashr: 9]


Miradi ya Hadithi