عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ المُغِيرَةِ، قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى المُغِيرَةِ رضي الله عنهما: اكْتُبْ إِلَيَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ، فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ ﷺ كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ: «لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ، وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلا يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ» وَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّه: «كَانَ يَنْهَى عَنْ قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةِ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ المَالِ، وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقُوقِ الأُمَّهَاتِ، وَوَأْدِ البَنَاتِ، وَمَنْعٍ وَهَاتِ».

Kutoka kwa Warad, Mwandishi wa Al-Mughirah, amesema:Muawiya alimwandikia Al-Mughirah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili:

1- Niandikie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na akamwandikia: 2- Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa akisema kila baada ya kila swala: “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja, Peke Yake, hana mshirika, ufalme ni wake, sifa njema ni zake, na Yeye ni Muweza wa yote. 3- Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kizuizi kwa ulichotoa wala mtoaji kwa ulicho kizuia. 4- Na hanufaishi mwenye utukufu, bali utukufu ni wako” 5- Na akamuandikia: “Alikuwa akiharamisha yaliyosemwa na kusengenya. 6- Kuuliza sana 7- Kupoteza pesa 8- Amekataza kuwaasi akina mama. 9- Mauaji ya watoto wachanga wa kike 10- Na kuzuia (kuwa na choyo) na kuchukua (kupenda kupewa)” .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole (101) Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa” .

[Al-Maidah: 101, 102]

Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima (23) Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni”.

[Al-Isra: 23, 24]

Na Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

 “Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana (88) Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi” .

[Ash-Shuaraa: 88, 89]

Na Akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

 “Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima” .

[Faatir: 2]

Na Akasema Mwenyezi Mungu

mtukufu Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari” .

[Qaaf: 18]

Na Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu :

" Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa (8) Kwa kosa gani aliuliwa”

[At-Takweer: 8, 9].

Miradi ya Hadithi