31 - MIONGONI MWA AINA ZA MAKADIRIO YALIYOTANGULIA

عن عبدِ الله بنِ مسعودٍ قال: حدَّثنا رسولُ الله ﷺ- وهو الصادقُ المصدوقُ -: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَبْعَثُ اللهُ إِلَيْهِ مَلَكًا بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ، فَيُكْتَبُ عَمَلُهُ، وَأَجَلُهُ، وَرِزْقُهُ، وَشَقِيٌّ أَمْ سَعِيدٌ، ثُمَّ يُنْفَخُ فِيهِ الرُّوحُ، فَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ، حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ، فَيَدْخُلُ الجَنَّةَ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ، حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَاإلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ، فَيَدْخُلُ النَّارَ» متفق عليه



Kutoka kwa Abdullah bun Masood, amesema: alitwambia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) – na yeye ndiye mkweli anae kubalika -

1.Hakika mmoja wenu hukaa katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha anakuwa pande la damu kwa siku nyinge kama hizo, kisha anakuwa pande la nyama kwa siku nyingine kama hizo 2.Kisha Mwenyezi Mungu anamtuma malaika kwa ajili ya mambo manne, aandike matendo yake, kifo chake, riziki yake na atakuwa mwema au muovu 3.Kisha anapuliziwa roho. 4.Kwa hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Motoni mpaka inabaki baina yake na kuingia Motoni kiasi cha dhiraa urefu wa mkono kutoka kwenye kiganja mpaka kwenye kiwiko, mipango ya Mwenyezi Mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Peponi, aningia Peponi. 5.Na hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi mpaka inabaki baina yake na kuingia Peponi kiasi cha dhiraa, mipango ya mwenyezi mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Motoni, anaingia Motoni” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu.




Muhtasari wa Maana

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ametaja katika hadithi hii baadhi ya hatua za ukuwaji wa kijusi katika tumbo la mama, kupuliziwa roho na kuandikiwa mambo yake yote. Kisha akabainisha kwamba kinacho zingatiwa katika matendo yake ni mwisho, mwenye kuhitimisha uhai wake kwa matendo ya watu wa Peponi, basi atakuwa miongoni mwao, na mwenye kuhitimisha uhai wake kwa matendo ya watu wa Motoni, basi atakuwa miongoni mwao.

Miradi ya Hadithi