عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ عِنْدَهَا، وَأَنَّهَا سَمِعَتْ صَوْتَ رَجُلٍ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِ حَفْصَةَ، قَالَتْ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذَا رَجُلٌ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِكَ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «أُرَاهُ فُلاَنًا»، لِعَمِّ حَفْصَةَ مِنَ الرَّضَاعَةِ، قَالَتْ عَائِشَةُ: لَوْ كَانَ فُلانٌ حَيًّا - لِعَمِّهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ - دَخَلَ عَلَيَّ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ؛ الرَّضَاعَةُ تُحَرِّمُ مَا تُحَرِّمُ الوِلادَةُ» 

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, mke wa Mtume, rehma na amani zimshukie:

1-    Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa kwa Aisha, na Aisha akasikia sauti ya mtu akibisha hodi katika nyumba ya Hafsa, : Akasema: Huyu mtu anabisha hodi nyumbani kwako, basi Mtume rehma na amani zimshukie akasema: “Ninamuona ni mtu Fulani ” kwa ami yake Hafsa kwa kunyonya sehemu moja. 2. Aisha akasema: unasemaje lau fulani angekuwa hai - ami yake kwa kunyonya – akaja nyumbani kwangu? Naye akasema: Ndiyo. Kunyonyesha kunayaharamisha yote yaliyoharamishwa kutokana na nasaba na kuzaa”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya”.

[An-Nisa: 23]

Miradi ya Hadithi