عَنْ أَبِي ذَرٍّ، عَن النَّبِيِّ ، فِيمَا رَوَى عَن اللهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَنَّهُ قَالَ: «يَا عِبَادِي، إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي، وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا؛ فَلا تَظَالَمُوا. يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ ضَالٌّ إِلَّا مَنْ هَدَيْتُهُ؛ فَاسْتَهْدُونِي أَهْدِكُمْ. يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ جَائِعٌ إِلَّا مَنْ أَطْعَمْتُهُ؛ فَاسْتَطْعِمُونِي أُطْعِمْكُمْ.يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ عَارٍ إِلَّا مَنْ كَسَوْتُهُ؛ فَاسْتَكْسُونِي أَكْسُكُمْ. يَا عِبَادِي، إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ، وَأَنَا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا؛ فَاسْتَغْفِرُونِي أَغْفِرْ لَكُمْ. يَا عِبَادِي، إِنَّكُمْ لَنْ تَبْلُغُوا ضَرِّي فَتَضُرُّونِي، وَلَنْ تَبْلُغُوا نَفْعِي فَتَنْفَعُونِي. يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، كَانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ مِنْكُمْ، مَا زَادَ ذَلِكَ فِي مُلْكِي شَيْئًا.يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، كَانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ، مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكِي شَيْئًا. يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، قَامُوا فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ فَسَأَلُونِي، فَأَعْطَيْتُ كُلَّ إِنْسَانٍ مَسْأَلَتَهُ، مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِمَّا عِنْدِي إِلَّا كَمَا يَنْقُصُ المِخْيَطُ إِذَا أُدْخِلَ البَحْرَ. يَا عِبَادِي، إِنَّمَا هِيَ أَعْمَالُكُمْ أُحْصِيهَا لَكُمْ، ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إِيَّاهَا، فَمَنْ وَجَدَ خَيْرًا فَلْيَحْمَدِ اللهَ، وَمَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذَلِكَ فَلا يَلُومَنَّ إِلَّا نَفْسَهُ».

Kutoka kwa Abuu Dharri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), aliyo yapokea kutoka kwa mola wake Mtukufu, hakika yeye amesema:

 “Enyi waja wangu, hakika mimi nimejiharamishia dhuluma, na nikaifanya kuwa haramu baina yenu, basi msidhulumiane.Enyi waja wangu, nyote mmepotea, ila niliye muongoza, basi niombeni uongofu, nami nitawaongoza.Enyi waja wangu, nyote mnanjaa ila niliye mpatia chakula, basi niombeni chakula, nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, nyote mko uchi, ila niliye mvisha, basi niombeni mavazi nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana, na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitawasamehe.Enyi waja wangu, hakika nyinyi hamuwezi kufanya juhudi za kunidhuru, mkanidhuru, na hamuwezi kufanya juhudi za kuninufaisha, mkaninufaisha.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye mcha Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo haliongezi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye muasi Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo halipunguzi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakisimama katika uwanja mmoja, wakaniomba, nikampa kila mmjo alicho kiomba, hilo halipunguzi chochote kwa nilivyo navyo, ila ni kama kiasi cha sindano inapo ingizwa baharini. Enyi waja wangu, hayo ni matendo yenu ninayadhibiti, kisha nitawalipa. Atakae pata kheri, basi amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakae pata kinyue asimlaumu yeyote zaidi yake mwenyewe”

Abuu Dharri Jundubu bun Junaadah, ukoo wa Ghifaari

Ni Abuu Dharri Jundubu bun Junaadah, ukoo wa Ghifaari, aliye ipa nyongo Dunia na msema kweli. Ni katika maswahaba wakubwa na walio bora. Miaka mitatu kabla Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) hajatumwa alikuwa akiabudu, anasimama usiku kusali. Alisilimu wanzoni kabisa, mpaka inasemekana kwamba ni wa nne kusilimu, aliondoka baada ya kifo cha Abuu Bakar kuelekea Shaam, akaishi huko mpaka Uthman alipo kuwa kiongozi ndio akamuita na kumuagiza akaishi Zabada, na akafia huko. Aliye ongoza ibada ya kumsalia aliku ni Abdullah bun Umar (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake).

Miradi ya Hadithi