عن ابنِ عمرَ رضي الله عنهما، أن رسول الله  ﷺ قال: «صلاةُ الجماعةِ أفضَلُ من صلاةِ الفَذِّ بسَبعٍ وعشرينَ دَرجةً»

Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema:

“Swala ya jamaa ni bora zaidi kuliko swala ya mtu pekee kwa daraja ishirini na saba.’’

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni (36) Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka (37) Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu”

[An-Nur: 36-38].

Miradi ya Hadithi