19 - KUMPENDA MTUME NA YANAYOFUNGAMANA NA HAYO

عَن أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضى الله عنه، قَالَ: بَيْنَمَا أَنَا وَالنَّبِيُّ ﷺ خَارِجَانِ مِنَ المَسْجِدِ، فَلَقِيَنَا رَجُلٌ عِنْدَ سُدَّةِ المَسْجِدِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «مَا أَعْدَدْتَ لَهَا؟»، فَكَأَنَّ الرَّجُلَ اسْتَكَانَ، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا أَعْدَدْتُ لَهَا كَبِيرَ صِيَامٍ، وَلا صَلاةٍ، وَلا صَدَقَةٍ،وَلَكِنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ، قَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». 


Kutoka kwa Anas bin Malik (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

Wakati mimi na Mtume (Rehma na Amani zimshukie) tunatoka msikitini tulikutana na mtu mmoja kwenye uwanja wa msikiti, (sehemu ya mbele) akasema (yule mtu): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Qiyama ni lini?Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akasema: “Umeandaa nini kwa ajili yake?”Mtu alikuwa huyo kana kwamba amekata tamaa.akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijajiandaa kwa funga nyingi, swala, wala sadaka.Lakini mimi nampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.Akasema Mtume (Rehma na Amani zimshukie): «Wewe utakuwa pamoja na uwapendao (siku ya kiama)


  1. Anas bin Malik (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) anasimulia kuwa wakati akitoka msikitini akiwa Pamoja na mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) walikutana na mtu mmoja mbele ya msikiti, mtu huyo akamuuliza Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) wakati wa kusimama qiyama. inasemekana kuwa mtu huyo ndiye yule Bedui aliyekojoa msikitini kabla ya hapo, jina lake anaitwa Dhul-Khuwaisrah Al-yemeni[1].

2.   Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimuondoa katika swali lake na kumuelekeza katika swali muhimu zaidi, ambalo ni: Je, umetayarisha nini kwa ajili ya Qiyaamah? Je, umeandaa ibada nyingi kwa ajili ya siku hiyo?

Makusudio ya Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) katika swali hili ni kumzindua mtu huyu ili atambue wajibu wake na ajue yanayompasa kufanya, nayo ni kujiandaa kwa ajili ya siku ya hesabu kwa kutenda matendo mema yatakayokuwa sababu ya kuingia Peponi, na sio lazima kujua wakati wa kusimama Kiyama, japo kuwa ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua wakati wake.

3.   Yule mtu aliposikia swali la Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) nyenyekea na kutulia, akatathimini matendo yake na akayaona ni machache saana, akakiri mapungufu yake, na kuomba msamaha kwa kuuliza swali hilo.

4.   Kisha akaeleza kwamba hakujitayarisha kwa kufanya ibada kubwa, japo kuwa ibada za Sunnah na utiifu zinazomuingiza mtu peponi na kumuepusha na moto ni nyingi saana, lakini mtu huyu inaonekana alitosheka kufanya matendo faradhi ambayo Muislamu lazima ayafanye[2].

Na inaweza kuwa alisema hivyo kwa sababu ya unyenyekevu wake na kuogopa kujitangaza, au Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimuona hafanyi ibada kwa wingi, au alimaanisha kwamba ibada zote ziko chini zikilinganishwa na upendo wake wa dhati kwa Mungu na Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake), jambo ambalo hakuna ibada kubwa inayolingana na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

5.   Hata hivyo, kubwa kuliko yote aliyoyaona yule Mtu katika matendo ambayo yatamnufaisha Siku ya Kiyama: ni mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na maana yake ni kuwa na mapenzi ya dhati ambayo athari zake zinahitaji utiifu kwa mambo mengineyo.

6.   Ndio maana Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimwambia ikiwa atakuwa na nia thabiti katika mapenzi yake, kwa kutekeleza masharti yake, basi atakuwa sambamba na ampendaye, maaana yake atakuwa sambamba na Mtume na maswahaba zake katika Pepo ya juu kabisa. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapo pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na (wakweli) wasadikishaji, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao”

[An-Nisa: 69].

Na ndio maana Anas (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alisema: “Nampenda Mtume na Abu Bakar, na Umar, na ninatarajia kuwa pamoja nao kwa sababu ya mapenzi yangu kwao, hata kama sijafanya kama waliyofanya.

Mafunzo

  1. Wazazi wa Anas na yeye pia hawakujali katika kumtumikia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) haliyakuwa si mtumwa, na kazi ya utumishi kwa wakati huo ilikuwa ni kazi ya watumwa, si kwa Watoto wa waheshimiwa, pamoja na hayo mama wa Anasi alimshika na kumpeleka kwa Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) ili amtumikie. Na hapo tunajifunza kuwa desturi na maneno yanayosemwa kwa watu yasimzuie Muislamu kufanya matendo ya kumuingiza peponi kama anasi alivyomuhudumia Mtume bila kujali maneno ya watu. 

  2. Anas (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alipenda sana kushikamana na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na kumtumikia licha ya umri wake mdogo, ndo maana zimekuja Hadith zikieleza kwamba Anasi alikuwa anacheza na vijana wenzake [3] wakati huo, hivyo basi tunajifunza kuwa si lazima katika kumlea kijana mdogo katika tabia njema kwa kumzuia mambo ambayo yanaendana na umri wake.

  3. Yule mtu alieuliza kuhusu wakati wa Qiyama, Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) hakujibu, bali alielekeza swali lake katika swali jingine lenye maslahi ya muulizaji na wengineo, na swali hilo lilihusu kutenda matendo mema kwa ajili ya siku ya kiama, na hii mbinu aliyoitumia Mtume inajulikana kwa wataalamu wa fasihi kama mbinu ya wenye hekima, ambayo mtu hujibu swali kwa faida ya muulizaji, na hiyo inamuongezea muulizaji faida ambayo hakuwa anajua. Kama jibu la Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwa mtu aliyemuuliza kuhusu kutawadha maji ya bahari, Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alimjibu kuwa “Maji yake ni safi, na mzoga wake ni halali kuliwa[4]”; katika sentensi hii Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alitoa ufafanuzi juu ya usafi wa maji ya bahari kwa ujumla, kisha akawaongezea kwamba mizoga ya bahari inajuzu[5]. Hivyo basi ni wajibu kwa Mlinganiaji na mwalimu achunge mahitaji ya watu, na atumie hekima katika maneno na majibu yake, asijibu tu kulingana na maswali yao, bali azungumze na watu kuhusu mambo yatayo wasaidia kidini na kidunia, pasina kuleta fitina, kwa kujibu kulingana na matakwa yao, ikiwa atafanya hivyo itakuwa hakuna faida katika ujuzi wake.

  4. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliigeuza fikra ya muulizaji kutoka katika maswali Yasiyo na tija kwake, ambayo hayana faida kujibiwa: (Qiyama kitasimama lini) kwenda hatua ya kivitendo: (Umetayarisha nini kwa ajili yake), ndio maana Imam Malik hakupenda kuzungumza maneno bala matendo, na ndivyo walivyokuwa wanachuoni wa kabla yake[6], na watu wengi hivi sasa katika mradi mbalimbali huzozana na kutofautiana katika mambo yasiyo na tija, hivyo basi ukiuliza uliza swali lenye faida.

  5. Vizuri Muislamu ayafanye maneno haya: “Umetayarisha nini kwa ajili ya Qiyama?” Kuwa ndio mfumo wa maisha yake, afanye hima kuwajibika kila siku kwa kufanya matendo mema, ili kuona namna ya kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu siku hiyo? Je, atakutana naye akiwa amemridhia au amemkasirikia?

  6. Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), sio tu kwa madai na kusema tu, bali ni hisia ya Moyo, Kisha inafuata kupata radhi za anaependwa na kumtii. kulingana na Upendo uliopo moyoni, kiasi kwamba Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kutafikia hatua ya kuwa zaidi ya pesa, watoto, na watu wote. Hivyo basi Anayedai kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi ajipime mwenyewe je anapata ushahidi wa mapenzi yake? Amesema Hassan Al-Basri: Baadhi ya watu walidai kuwa wanampenda Mwenyezi Mungu, basi akawajaribu kwa aya hii[7]:

    “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi. Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu”

    [Al Imran: 31].

  7. Haijalishi unadhambi kiasi gani moyoni mwako, au unafanya madhambi kiasi gani katika Maisha yako, Kwa hivyo usiache kumpenda na kumtukuza Mwenyezi Mungu pamoja na kumpenda Mtume, Rehema na Amani ziwe juu yake, kwani sisi sote hatufikii nafasi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu peponi; Kwa sababu ya Daraja zao kubwa, na Ukubwa wa Ibada zao, na ukweli wa Imani zao na Utiifu, licha ya mateso na misukosuko waliyopitia. Pamoja na hayo yote tunaweza kuwa pamoja nao huko peponi kwa kuwapenda vyema, na kuwaheshimu, na kufuata mienendo yao, na kutanguliza upendo wao kuliko upendo wa watu wote.  Na hii Ni bishara njema kwa wale walio makini. Ndio maana Anas (Mwenyezi Mungu amuwie Radhi) akasema: “Sikupata kuwaona Waislamu wakifurahi zaidi baada ya Uislamu kwa kitu kingine kama walivyofurahia kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake” .

8.    Jitahidini kumpenda zaidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), kwa kufanya sababu za kupata upendo huo, kama vile kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumswalia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na kuusafisha moyo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuzikumbuka neema zao, na kuwatii kama unavyoona mpenzi anatafuta Radhi za kipenzi chake, mapenzi yako kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, rehema na amani ziwe juu yake, Yawe makubwa Zaidi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

“Na miongoni mwa watu wapo wanao abudu Waungu wasiokua Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama wanavyompenda Mwenyezi Mungu, lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi.”

[Al-Baqarah: 165]

Marejeo

  1. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (10/555).
  2. Tazama: Al-Mufhim cha Al-Qurtubi (6/646).
  3. Imesimuliwa na Muslim (2604).
  4. Imepokewa na Al-Tirmidhiy No. (69).
  5. Tazama: Al-Kawakib Al-Dariri cha Al-Karmani (22/35).
  6. Tazama: “"Jamie Bayn Aleilm Wafadlihi"” ya Ibn Abd al-Barr (2/95).
  7. "Tafsir Ibn Kathir" (2/32), ambayo Aya imetajwa hapa.


Miradi ya Hadithi