عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ:«الإِيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ - أَوْ: بِضْعٌ وَسِتُّونَ - شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإِيمَانِ» متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimfikie):“Imani ina daraja sabini na kitu, au sitini na kitu.Daraja bora zaidi ni kusema: Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu.Na daraja la chini kabisa ni kuondoa maudhi njiani.Na haya (aibu) ni daraja katika daraja za Imani.” Hadithi hii Imepokelewa na Imam Bukhari Na Muslimu.

Imepokewa na Al-Bukhari (9) na Muslim (35),

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana



Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi”

[Al-Anfal: 2].

Amesema allah mtukufu: 

“Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi (124) Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ni makafiri” (125)

[At-Tawbah: 124, 125].

 

Na amesema mtakatifu: 

“Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwambahapana    mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu”

[Al Anbiyaa: 25].

Pia amesema Allah Mtukufu 

 “Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima”

[Al-Fath: 4]

Miradi ya Hadithi