عن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه  عَنِ النَّبِيِّ قَالَ: «إِذَا اقْتَرَبَ الزَّمَانُ، لَمْ تَكَدْ رُؤْيَا الْمُسْلِمِ تَكْذِبُ، وَأَصْدَقُكُمْ رُؤْيَا أَصْدَقُكُمْ حَدِيثًا، وَرُؤْيَا الْمُسْلِمِ جُزْءٌ مِنْ خَمْسٍ وَأَرْبَعِينَ جُزْءًا مِنَ النُّبُوَّةِ، وَالرُّؤْيَا ثَلَاثَةٌ: فَرُؤْيَا الصَّالِحَةِ بُشْرَى مِنَ اللهِ، وَرُؤْيَا تَحْزِينٌ مِنَ الشَّيْطَانِ، وَرُؤْيَا مِمَّا يُحَدِّثُ الْمَرْءُ نَفْسَهُ، فَإِنْ رَأَى أَحَدُكُمْ مَا يَكْرَهُ، فَلْيَقُمْ فَلْيُصَلِّ، وَلَا يُحَدِّثْ بِهَا النَّاسَ»


Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, amesema:

“Qiyama kitakapokaribia, ndoto ya Mwislamu haitakua uongo. Mwenye ndoto za kweli zaidi katika nyinyi ni yule msema kweli katika mazungumzo Ndoto ya Muislamu ni sehemu moja kati ya sehemu arobaini na tano za utume. Kuna aina tatu za ndoto: ndoto njema ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Ndoto ya huzuni kutoka kwa Shetani. Na Ndoto kutokana na yale yanayompata mtu moyoni mwake. Akiona mmoja wenu jambo ambalo analichukia basi na asimame na aswali wala asiwaambie watu jambo hilo.”

Muhtasari wa Maana

Kiyama Kikikaribia, njozi anazoziona Muislamu zitakuwa za kweli zaidi, na kadiri mtu anapokuwa msema kweli ndivyo Ndoto zake zinakuwa za kweli zaidi. Ndoto nzuri ni moja ya sifa za unabii, na kuna aina tatu za Ndoto; Habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, huzuni kutoka kwa Shetani, na mazungumzo ya kibinafsi. Mtu akiona kitu anachokichukia katika ndoto, basi na atie udhu na aswali kiasi anachotaka, na asimwambie yeyote kuhusu hilo, kwa sababu halimdhuru.

Miradi ya Hadithi