عَنْ أَنَسِ بْن مَالِكٍ رضي الله عنه، أَنَّ النَّبِيَّ قَالَ: «كُلُّ ابْنِ آدَمَ خَطَّاءٌ، وَخَيْرُ الخَطَّائِينَ التَّوَّابُونَ»

Kutoka kwa Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume Swalla Allaahu alayhi wasallam amesema: 1- “Kila mwana wa Adamu ni mwenye dhambi. 2- Na wabora wa wakosefu ni wale wanaotubu”.


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu utukufu ni wake: “Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua”

[Al Imran: 135].

Na akasema pia Allah aliyetukuka: “Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima”.

[An-Nisai: 17]

Na akasema pia Allah aliyetukuka: “Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”

[Al-Furqan: 70]

Na akasema pia Allah Mtukufu: “Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu (53) Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa” . 

[Al-Zumar: 53, 54]

 Na akasema pia Allah Mtukufu: “Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua mnayo yatenda”.

[Al-Shura: 25]



Miradi ya Hadithi