عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ «مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيَا، نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ يَسَّرَ عَلَى مُعْسِرٍ، يَسَّرَ اللهُ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا، سَتَرَهُ اللهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَاللهُ فِي عَوْنِ الْعَبْدِ مَا كَانَ الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ،  وَمَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْمًا، سَهَّلَ اللهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ،  وَمَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ، يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ، وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمِ السَّكِينَةُ، وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ، وَذَكَرَهُمُ اللهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ، وَمَنْ بَطَّأَ بِهِ عَمَلُهُ، لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ».

Kutoka kwa Abu Hurayrah, amesema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie amesema: 1. “Mwenye kumuondolea Muumini dhiki za kidunia, Mwenyezi Mungu atamwondolea moja ya dhiki za Siku ya Kiyama. 2. Na mwenye kumfanyia wepesi aliyesongwa na mambo, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na akhera. 3. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. 4. Na Mungu humsaidia mja maadamu mja anamsaidia ndugu yake. 5. Na anaye pita njia kwa ajili ya kutafuta ilimu, Mwenyezi Mungu atamsahilishia njia ya kwenda Peponi. 6. Kila watu wanapokusanyika katika moja ya nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu. na wakisomeshana wao kwa wao, amani huwashukia. Na rehema huwafunika, Malaika huwazunguka, na Mwenyezi Mungu huwataja miongoni mwa walio pamoja Naye. 7. Na mwenye kucheleweshwa na vitendo vyake, nasaba yake haitamharakisha.”]



Muhtasari wa Maana

Mtume rehma na amani zimshukie anaeleza juu ya wema wa kuwasaidia watu katika mambo yao ya kidunia, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humsaidia mja kwa kumsaidia ndugu yake, kisha akataja fadhila ya kutafuta elimu, na kheri anazozipata mtafuta elimu kama vile amani na rehema, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtaja kwa Aliye Juu. Kisha akaonyesha kwamba jambo la maana ni biashara, si ukoo.

Miradi ya Hadithi