عن أبي هريرة قال: قال رسول الله ﷺ: قال اللهُ - عزَّ وجلَّ -: «الكِبْرياءُ رِدائي، والعَظَمةُ إزاري، فمَن نازَعَني واحدًا منهما، قَذَفْتُه في النارِ».


Kutoka kwa Abu Said na Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie): 

1. “Utukufu ni vazi lake, 

2. Kiburi ni shuka lake, 

3. Basi mwenye kuninyang’anya vazi hilo nitamuadhibu.”


Mtume (Rehma na Amani zimshukie) anasimulia kuhusu Hadith hii aliyoteremshiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba:

1- Utukufu unaashiria maana ya kutawaliwa, kutawala, nguvu, na utukufu wa majina na sifa, na sifa hizi ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, kwa sababu hakika Yeye anastahiki sifa zake, nazo ni kama vazi. Vazi hilo kwa mtu ni vazi linalofungwa katikati na kusitiri sehemu ya chini ya mwili wake, hivyo uhalisia wake ni kwamba hilo vazi ni stara na miliki mahsusi ya mmiliki wake, na ni kizuizi chake baina yake na viumbe wengine, hakuna wa kumnyang’anya. Utukufu ni sifa ambayo Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayo mwenyewe, hivyo hakuna kiumbe mwenye haki ya kushirikiana na Mwenyezi Mungu, hivyo Mwenyezi Mungu anajivuna na kujitukuza juu ya watu.
2- Kiburi kinaashiria mtu kujinyanyua juu ya wengine, na kujiona mbora zaidi na mwenye heshima juu yao. Na sifa hiyo hatakiwi kuwa nayo mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, kwa sababu anastahiki sifa zake, hivyo ni kama vazi, na vazi la mtu ni vazi linalowekwa juu ya mabega yake ili kusitiri sehemu ya juu ya mwili wake. Uhalisia wake ni kama stara na mali inayomilikiwa na mhusika, na ni kizuizi baina yake na wengine pia, kwa hivyo hakuna mzozo juu yake.
Miongoni mwa yanayobainisha maana ya Hadithi hiyo ni riwaya mashuhuri kutoka kwa Hadithi ya Abu Hurairah kutoka kwa Mtume Rehema na Amani zimshukie

ambaye amesema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Mtukufu: Kiburi ni vazi langu, na ukuu ni nguo yangu, basi anayechukua sifa moja katika hizo Nitamtupa motoni” [1]

, na tafauti baina ya kiburi na utukufu: ni kwamba mwenye kiburi anakuwa na sifa ya kiburi; Ndio maana Mtume amani iwe juu yake alipoeleza kiburi, alisema: “Kiburi ni kuiacha haki, na kuwadharau watu [2].Yaani kuwadharau.Ama anayejitukuza huwa anaona kuwa amekamilika mwenyewe, hata bila kujinyanyua juu ya wengine, na kujitukuza huko ndio kunatafsiriwa kwa maana ya kujipenda [3], Kwa hiyo, kiburi kinakuwa juu zaidi kuliko kujifakhiri na majivuno, Mwenyazi Mungu anakifananisha na vazi. Akafananisha kujikweza na nguo inayo valiwa katikati ya mwanadamu kuteremka chini, na hii ndio nguo inayovaliwa juu ya nguo na nyengine huvaliwa chini.
3- Mwenye kutaka kushirikiana na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika sifa hizi kwa kuwafanyia watu kiburi na kutakabari juu ya watu, Mwenyezi Mungu atamtia Motoni na kumwadhibu humo. Kwasababu Kiumbe yeyote haipaswi kuwa na sifa hizi; Kwa sababu sifa ya kiumbe ni unyenyekevu na utiifu [4], Mwenyezi Mungu Mtukufu amekataza waja wake kufanya kiburi katika ardhi na kujisifu

kwa hivyo akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima”. 

[Al-Isra: 37]

Na akaelezea kuwa aliufanya moto kuwa mwisho wa wafanyao kiburi, wapotovu

akasema:

Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanao fanya kiburi” .

[Al-Zumar: 60]


1- Onyesha ukweli kwa uwazi na uzuri kadiri uwezavyo, Kwa hivyo tazama matumizi ya tashibiha na viwakilishi vya balagha katika Hadith Qudsi vinavyobainisha maana na kuzileta karibu. Wahubiri, Walinganiaji na wasomi wanapaswa kutumia njia hizo.
2- Je, tunajichunga ili kuona: Je, Tunajitukuza juu ya wengine? Pengine kama mtu angejinasibu, huwenda mwanadamu akijichunguza ili kuona kama ana kiburi juu ya nafsi yake na ana kiburi juu ya wengine. Ama kwa sababu ya pesa, cheo, ujuzi, mamlaka, cheo cha kijamii, au jambo lingine lolote, atamdharau mgeni, maskini, watu, au kitu kingine chochote.
3- Sio katika kiburi na sio kujitukuza mtu kujiweka vizuri katika mandhari yake na kujiremba

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud Mwenyezi Mungu amuwiye radhi kutoka kwa Mtume, amani iwe juu yake, amesema:

“Mwenye uzito wa chembe ya kiburi moyoni mwake hataingia Peponi.” Mtu mmoja akasema: Mtu anapenda nguo zake ziwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri? Akasema: "Mungu ni mzuri na anapenda uzuri, kiburi ni kuipinga haki, na kuwadharau watu" [5]

Ujeuri ulioharamishwa ni kuikanusha haki na kujivuna, na kuwadharau watu.
4- Utukufu wa Mwenyezi Mungu uwe ndani ya nyoyo zetu, na ndimi zetu na mikusanyiko yetu, na tuifute kwa hayo majivuno ya nafsi.” Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifanya takbira kwa kusema. (Mwenyezi Mungu ni mkubwa) ni alama ya swala, mwito wa kuswali, na sikukuu, na ilikuwa yenye kutamanika katika sehemu za juu kama vile Al-Safa na Al-Marwah, na ikiwa mtu aliinuka kwa heshima au akapanda mnyama na kadhalika. Imeelezwa kuwa moto huo unazimika nayo, hata ukiwa mkubwa, na wakati wa mwito wa kuswali, Shetani hukimbia [6].
5- Tafakari juu ya udhaifu wako kutokana na kutambua maslahi yako, na kutokana na kuweza kuyafikia, na kwamba nyingi katika hizo ni sababu ambazo haziko mikononi mwako. Na kwamba unaona rai leo na kesho unaifanyia mzaha, na unaona uwezo wa kufanya jambo fulani, na unaizuilia kwa ufahamu zaidi wa sababu, na kwa hayo unajua kuwa Mwenyezi Mungu ameharamisha tu kiburi kwa sababu ni sifa ya Mwenyezi Mungu. Kiumbe ambaye sifa yake ya ukaidi na unyonge si kuwa na kiburi ; Kwa ajili hiyo, Sharia inakataza mtu kuwa na sifa hizi mbili. na ikayafanya kuwa miongoni mwa madhambi makubwa; Kwani anaye dhania ukamilifu wa nafsi yake, na akasahau neema za Mwenyezi Mungu katika yale aliyoyafanya kuwa mahsusi. Aatakuwa hajitambui nafsi yake na Mola wake, nayo ni sifa ya Iblis inayombeba kwa kauli yake:

“Mimi ni bora kuliko yeye” .

[Al-A’raf: 12]

Na ni Ufafanuzi wa Firauni anayembeba unatokana na kauli yake:

{Mimi ni Mola wenu Mtukufu} .

[Al-Naza’at: 24]

Malipo yao yalikuwa kwamba wao ndio walioadhibiwa vikali zaidi miongoni mwa watu wa Motoni [7].
6- Baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu hupenda kujulikana na kupambwa na waja wake, kama vile rehema, msamaha, ukarimu na kadhalika. Kwa sababu ziko katika ukamilifu wao wa asili, hivyo mtu akizitafuta, anatafuta ukamilifu, na baadhi ya sifa ni mahususi kwa Mwenyezi Mungu. Na akawakataza waja wake kusifika kwa sifa hizo kama vile kiburi na ukuu, kwa sababu ni kheri pale mwenye nayo atakapokamilika, na akidai kuwa nayo mtu asiyestahiki, inakuwa ni batili.
7- Mtu anatakiwa kujiweka mbali na kiburi na kujitukuza, na avunje matamanio yake hayo kila anapopata kitu katika dunia hii; Nazo ni miongoni mwa sifa zinazo mwajibisha mja kuingia motoni.Sufyan bin Uyaynah – Mwenyezi Mungu amrehemu – amesema: “Yeyote aliyemuasi kwa matamanio, basi tafadhali tubu kwa ajili yake, kwani Adam – amani iwe juu yake – aliasi kwa kufanya matanio yake, akasamehewa. Ikiwa maasi yanafungamana na kiburi, basi muhofie mtu huyo kuwa atalaaniwa; kwa sababu Ibilisi aliasi kwa maasi yaliyo fungamana na kiburi, alilaaniwa."[8]
8- jaribu kurekebisha kiburi chako mwenyewe kwa kuitahadharisha kinyume cha nia yake; Mwenye kiburi anapojiona kuwa mkubwa. Mwenyezi Mungu humuadhibu kwa kinyume cha dhamira yake kama vile kumuadhibu kwa unyonge, udogo, na ubaya.

Anasema Mtume rehma na aamani zimshukie:

“Watafufuliwa wenye kiburi Siku ya Kiyama kama atomu katika picha za watu, na fedheha itawafunika kila mahali.”[9]

Na Mwenyezi Mungu anaweza kuwaadhibu hapa duniani kabla ya Akhera, kama ilivyokuwa kwa Qarun pale Mwenyezi Mungu alipomdidimiza aridhini. Na Firauni alipomzamisha.

Kutoka kwa Abu Hurairah, kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema:

“Na mtu alipokuwa akitembea kwa majivuno katika vazi lake, na nafsi yake ikampambia kufanya hayo na kujipenda, basi Mwenyezi Mungu akaiamrisha ardhi ikammeza, na anadidimia aridhini mpaka Siku ya Kiyama. [10]


9- Jichunguze katika mjadala wowote wa kielimu au kijamii, hapana shaka kiburi ni sababu kubwa mojawapo ya kukanusha haki. Na ndio sababu ya kuangamizwa kwa mataifa mengi yaliyopita; kutokana na jeuri yao ya kutomfuata Nabii ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwao.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu watu wa Nuhu:

“Na wakaendelea katika maasi na wakafanya jeuri na kiburi”.

[Nuhu: 7]

Na akasema Mwenyezi Mungu:

“Na Qaruun na Firauni na Haamana, bila shaka Musa Amani iwe juu yake aliwajia kwa hoja zilizo wazi, lakini walijivuna katika nchi, na wakafanya kiburi katika Ardhi, Na hawakuwa wa kwanza kuamini.”

[Al-Ankabut: 39]

na akasema Mwenyezi Mungu:

“Ama kina A'di walijivuna katika ardhi bila ya haki, na wakasema: Ni nani mwenye nguvu kuliko sisi” 

[Fussilat: 15]

Kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu aliunganisha mazungumzo juu ya kiburi chao kwa kueleza uharibifu wao; hivyo Muislamu lazima ajitahidi kuondoa kiburi na kujiona.
10- Mutrif bin Abdullah bin Al-Shakheer, Mwenyezi Mungu amrehemu, alimuona Yazid bin Al-Muhallab bin Abi Sufra akitembea kwa majivuno huku akiwa amevaa nguo ndefu ya kuburuza chini. Mutarrif akasema: Ewe Abdullah, huu ni mwendo ambao Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanauchukia. Yazid akasema: Hunijui?! Akasema: Nakujua. Mwanzo wako ni shahawa iliyorutubishwa, na wa mwisho wako ni mzoga wa kunuka, na baina yako unabeba uchafu. Kwa kauli hiyo alinyooka na kuacha kutembea kwake kwa kujidai na kuringa [11].
11- Mshairi akasema:
Ni mnyenyekevu kiasi gani mtu asiyejua = Kisha Unyenyekevu wake unasitiri ujinga wake
Na mtu pekee katika elimu yake = kiburi kinaharibu fadhila za elimu yake
Kwa hivyo acha kiburi muda wote unapoishi = - na usiwe rafiki na wenye kiburi 
Jeuri ni kasoro kwa mvulana = muda wote kiburi huharibu matendo mema.
12- Wengine wakasema:
Ewe rafiki, kiburi ni tabia mbaya = si chochote ila ni sifa ya watu wajinga.
Kujivuna ni ugonjwa ambao hauwezi kuponywa = mpaka kutokufa kupatikane duniani
Kwa hiyo teremsha bawa lako kwa watu, utawashinda = hakika unyenyekevu ni tabia ya wenye hekima.
Ikiwa mwezi unaong'aa ungejipenda = ungeuona ukishuka kuelekea vumbi

Marejeo

  1. Imepokewa na Abu Daawuud (4090) na Ibn Majah (4174).
  2. Imepokewa na Muslim (91).
  3.  Tazama: “almifham lamaa 'ashakil min talkhis kitab muslimin" cha Al-Qurtubi (1/286).
  4. Tazama: “Maalam al-Sunan” cha al-Khattabi (4/196).
  5. Imepokewa na Muslim (91).
  6. Majmuu’ al-Fatawa cha Ibn Taymiyyah (10/196).
  7. Tazama: “"Almifham Lamaa 'Ashakil Min Talkhis Kitab Muslimin"  cha Al-Qurtubi (1/287).
  8. “Tahdheeb al-Kamal fi Asma’ al-Rijal” cha al-Muzzi (11/191).
  9. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (2492).
  10. Imepokewa na Al-Bukhari (5789) na Muslim (2088), na maneno ni yake.
  11. “Vifo vya watu mashuhuri” cha Ibn Khalilkan (6/284), “Sir Al-Alam Al-Nubala” cha Al-Dhahabi (4/505).


Miradi ya Hadithi