عن أبي هُريرة رضي الله عنه:أن رسول الله ﷺ دخل المسجد فدخَل رجلٌ، فصلَّى، فسلَّم على النبيِّ ﷺ، فرَدَّ وقال: «ارجِعْ فصَلِّ؛ فإنَّكَ لم تُصَلِّ»،فرجَعَ يُصَلِّي كما صَلَّى، ثم جاء، فسلَّمَ على النبيِّ ﷺ، فقال: «ارجِعْ فصَلِّ؛ فإنَّكَ لم تُصَلِّ» ثلاثًا، فقال: والذي بعَثَكَ بالحقِّ ما أُحسِنُ غَيرَه، فعَلِّمْني، فقال: «إذا قُمْتَ إلى الصلاةِ فكَبِّرْ،ثم اقرَأْ ما تَيسَّرَ معَكَ منَ القرآنِ، ثم اركَعْ حتى تَطمئِنَّ راكعًا، ثم ارفَعْ حتى تَعدِل قائمًا، ثم اسجُدْ حتى تَطمئِنَّ ساجِدًا، ثم ارفَعْ حتى تَطمئِنَّ جالسًا، وافعَلْ ذلك في صلاتِكَ كلِّها»

Kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake  amesimulia kuwa:

1. siku moja Mtume aliingia Msikitini, akaingia mtu fulani akaswali, kisha akamsalimia Mtume Rehema na Amani zimshukie, akajibu salamu na kusema: “Rudi ukaswali kwani hukuswali.” 2. Akarudi akaswali vile alivyoswali mwanzoni, kisha akaja akamsalimia Mtume (saw), akasema: “Rudi ukaswali kwani hukuswali.” Mara tatu, akasema Mtu yule: “Naapa kwa yule aliyekutuma kwa haki, mimi sifahamu kufanya vizuri kuliko hivi, basi naomba unifundishe. 3. Akasema Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) : “ukisimama kwa ajili ya Swala, basi toa takbira. 4. kisha soma aya nyepesi kwako katika Qur’ani . 5. Kisha rukuu mpaka utulizane katika rukuu, kisha inuka mpaka usimame sawasawa, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha inuka mpaka utulie katika kikao, na ufanye hivyo katika Swala yako yote


Hadith hii ni moja ya hadithi muhimu sana juu ya sheria ya Swala, kwani imejumuisha nguzo na wajibu muhimu zaidi za swala, na wanazuoni wa sheria waliizingatia sana hadithi hii na wakaitumia kama ushahidi katika mambo mengi ya sheria, na ni mashuhuri sana kwa wanachuoni kama: “Hadithi ya mwenye kuswali vibaya. ”

1. Mtu mmoja aliingia msikitini akaswali, na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa akitazama swala yake, mtu huyo alipomaliza kuswali akaja kwa Mtume (saw). na akamsalimia, kisha Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamuamrisha kurudia na kwamba swala yake haijakubaliwa  wala haifai.

Na lau ingelikuwa inafaa, asingelimuamrisha kurudia, bali angemtahadharisha tu na makosa aliyoyafanya ili kuyaepuka baada ya hayo.

2. Yule mtu akarudi na akaswali kama alivyoswali mara ya kwanza, na kwa sababu hiyo, aliporejea kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamuamuru arudie tena, basi yule mtu akaenda akaswali kama swala yake ya kwanza.  na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamuamrisha arudie, basi mtu huyo akamwambia kuwa haboreshi zaidi ya hiyo swala, na akamuomba Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) amfundishe kuswali, Na ni makosa gani aliyoyafanya, yaliyopelekea  akaharibu swala yake.

Mtume, Rehema na Amani zimshukie, hakumueleza alichokosea tangu mwanzo, labda kwa sababu Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake)  alidhani kwamba mtu huyo anazijua hukumu za swala, na wajibu wake na nguzo zake, lakini akakiuka elimu yake, hivyo akamuamuru kurudia, pale alipomwambia mtu huyo kwamba haboreshi zadi ya hapo akamfafanulia hukumu zake, au huwenda ni kwa sababu yeye, amani iwe juu yake alidhani ikiwa atamuamrisha mtu huyo kurudia mara kwa mara, kisha akamueleza sababu ya yeye kumrejesha basi hiyo itasababisha kueleweka zaidi na asisahau Baada ya hapo kamwe. [1]

3. Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamwambia akitaka kuswali aanze na takbira ya kufungua swala. Maana yake ni kuwa ni nguzo ambayo bila hiyo swala haifai, kwani Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alimfundisha mtu yule yanayopelekea Swala yake iwe sahihi, na hii  ilikuwa sehemu ya kujifunza , si vyema kuongeza katika  nguzo Sunnah na mfano wa hayo.[2]Mtume sawa hakutaja nia kwa sababu mtu huyo aliijua; kwani Moja ya misingi ya dini ambayo hakuna asiyeijua ni kwamba matendo ni kwa nia, iwe Katika swala, zaka na ibada zote.

4. Kisha akamuamrisha asome yaliyo mepesi zaidi kwake katika Qur’ani, na hii haimaanishi kuwa inajuzu kwake kusoma chochote anachotaka, Bali mchanganuo wa hayo upo katika Hadiith nyingine kwamba ni wajibu. kusoma suratul fatiha na kwamba: “Hapana Swala kwa asiyesoma Suratul Fatiha ya kwa usahihi” [3]hivyo basi Kinachokusudiwa katika mepesi ndani ya Qur’an ni Al-Fatihah, Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewarahisishia kuihifadhi wanaume, wanawake na watoto, au kinachokusudiwa baada ya Al-Fatihah katika kisomo, kwani mtu yule alikuwa anajua kuwa kusoma Al-Fatihah ni nguzo ya Swala, ndio maana akamuelekeza kusoma yale yanayofuata ikiwa anaweza kufanya hivyo.[4]

5. Kisha Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) akamuamrisha arukuu na atulizane katika rukuu, na awe amenyooka wakati wa kuinuka, na atulizane katika kusujudu. Na makusudio ya maelekezo haya ni kubainisha kuwa kutulizana na kutokuwa na haraka katika swala ni moja ya nguzo za swala ambayo bila ya hiyo swala haisihi, na ndio maana akamuamrisha arudie tena. 

Na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) aliikosoa swala isiyo na utulivu, na akasema: “hiyo ni swala ya mnafiki; Hukaa na kulitazama jua hata likiwa baina ya pembe mbili za Shetani, hapo ndo anainuka na kuidonoa swala rakaa nne bila kumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake ispokuwa kidogo tu.[5]” Na Maana ya kudonoa ni: kuswali kwa kasi katika rakaa zote na kutokuwa na utulivu, kama anavyodonoa kuku.

Na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) ametaja katika hadithi hii baadhi ya nguzo za swala ambazo swala haikubaliki bila ya hizo, na akaziacha nguzo nyinginezo, kama: nia, kukaa katika tashahhud ya mwisho, na kutoa salamu; Kwa sababu mtu huyo alijua mambo haya, na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alimuona akiyafanya, lakini mambo mengine yalikuwa hayapo kwake, basi Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamfundisha kufanya yale aliyokuwa hayajui.[6]

MAFUNDISHO:

1.Hadithi hii imetupa faida kuwa Muislamu akiingia msikitini na akakuta kuna watu wamekaa ndani yake basi ni vyema kwake kuswali swala inayojulikana kama maamkizi ya  msikiti kwanza kisha awasalimie waliokaa.

2.Ni wajibu kwa Muislamu kujifunza elimu ya kisheria ambayo kwayo ibada yake hukubaliwa; Ili kutobatilisha ibada yake.

3.inapendeza kwa mwanachuoni, msomi na mjuzi wa sheria na mlinganiaji akae msikitini na watu wazoee kukusanyika kwake kwa ajili ya kujifunza dini yao, na akiwapa mawaidha na kuwahimiza kutenda mema, na kuwabainishia swala ya Mtume (saw) , kama ilivyo.

4.Ikhlas (yaani kumkusudia Allah) ni katika ibada na kumuiga Mtume katika sunnah zake ni sharti katika kukubaliwa matendo, kama ilivyo kukosa sharti la ikhlasi kunabadilisha matendo, vivyo hivyo kwenda kinyume na sunnah za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) hupelekea kutokubalika matendo hata kama nia ni njema. 

5.inafaa kwa mlinganiaji na msomi wa sheria kuchelewesha kubainisha jambo katika kikao cha kielimu kwa sababu maalumu; Kama vile kumfanya msikilizaji awe na shauku ya kusikia hukumu ya kisheria katika hilo jambo, au kupupia watu kukusanyika ili kusikia kutoka kwake, na kadhalika.

6. Hadithi hii inaashiria kuwa inapendeza kutoa salamu na ni wajibu kuitikia, na kwamba inapendeza kuirudia ikiwa mtakutana mara kwa mara, hata ikiwa muda mchache umepita, na kwamba ni lazima kuitikia kila wakati.

7.Katika Hadithi hii kuna ushahidi kwamba mwalimu inabidi awe mpole kwa wanafunzi na wasiojua, na kuwafundisha kwa utaratibu, na kuwabainishia masuala mbalimbali ye kielimu, na kufupisha makusudio, na kutosheka kwa kuwapa elimu kidogo kidogo, hasa kwa kuanza na mambo muhimu ambayo yanaweza kukaririka mapema, na kufanyiwa kazi.[7]

8.Ufunguo wa swala ni takbira, nayo inaashiria kwamba tayari umeshaingia kwenye swala kwa kusema: “Allah Akbar” yaan Mungu ni mkubwa,” ni haki ya kumfanya mkuwa kubwa kuliko dunia na vilivyomo ndani yake, hivyo basi hautakiwi kushughulishwa na dunia ukaacha unyenyekevu na utulivu katika swala. 

9. Hadithi hii inabainisha kuwa vizuri kuwafanyia uwepesi Waislamu na wala haikugawiwa kwa yale ambayo ni magumu kwao, basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamrisha mtu huyo kusoma katika lililo jepesi,hivyo ni  kinyume cha sheria kudumu kwa baadhi ya maimamu katika kusoma sura ndefu katika swala na kuwatilia uzito watu, na akasema: “ Pindi mmoja wenu akiwaswalisha watu basi aifanye nyepesi swala yake, Hakika miongoni mwao wapo walio dhaifu, wagonjwa na wazee, na ikiwa mmoja wenu ataswali pekeyake  basi na aifanye ndefu kiasi apendavyo.[8]”

10. Utulivu ni nguzo katika swala, bila ya utulivu swala si sahihi, na makusudio yake ni kuelewa maana ya anachokisema Muislamu ndani ya swala yake ,miongoni mwa nyiradi na dua, na sio harakati tu anazozifanya Muislamu. , kuinuka na kuinama.

11. Miongoni mwa kuusiana haki na kuamrisha mema na kukataza maovu, ni Pamoja na kuwahadharisha na kuwaelimisha wajinga

Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Wahab Allah amrehem amesema: Hudhaifa (ra) alimuona mtu hatimizi rukuu zake wala sujuud zake,akamwambia: Wewe hujaswali, na kama utakufa katika hali hii basi utakufa katika maumbile isiyokuwa yale ambayo Allah kamuumba Muhammad Rehma na amani ziwe juu yake. Na haya ni makemeo makali sana.[9]

12. Mshairi akasema:

Unasali sala sawa isiyokuwa na  moyo = inayo mfanya mtu astahiki kuadhibiwa.

Ole wako! Wajua ni nani unae msemesha hali ya kupuuza? =Na mbele ya yule unaye muinamia bila ya unyenyekevu? .

Unamsemesha kuwa wewe tu tunakuabudu hali ya kumuelekea=  mwenginewe  katika swala yako pasina dharura ya kufanya hivyo!.

Na kama angekujibu umsemeshae bila ya kukutizama= basi ungepasuka kwa hasira naghera juu yake.

Marejeo

  1. Tazama: “"Sharah Almushkat Alkashif Ean Haqayiq Alsanani"cha Al-Twibi (3/977), “Al-Tahdeh Lash-i-Sharh Al-Jami’ Al-Sahih” cha Ibn Al- Mulqin (30/313), “Fath Al-Bari” cha Ibn Hajar (2/281).
  2. Tazama: "'Iikmal Almuealim Bifawayid Muslimin"cha Qadhi Iyadh (2/282).
  3. Imepokewa na Al-Bukhari (756) na Muslim (394). Tazama: “Maalim Al-Sunan” cha Al-Khattabi (1/210), “"'Iikmal Almuealim Bifawayid Muslim” cha Al-Qadi Iyad (2/282),
  4. ““Al-Mufhim Limaa 'Ashakala Min Talkhis Kitab Muslimin" . ” cha Al-Qurtubi (2/29).
  5. Imepokewa na Muslim (622).
  6. Tazama: “sharh Al-Nawawi alaa Muslim” (4/ 107).
  7. sharh Al-Nawawi alaa Muslim (4/ 108, 109).
  8. Imepokewa na Al-Bukhari (703) na Muslim (467), kwa kutoka kwa Abu Hurairah (ra)
  9. Imepokewa na Al-Bukhari (791).


Miradi ya Hadithi