عن ابنِ عُمرَ رضي الله عنهما، أنَّ النبيَّ ﷺ قال: «عَلَى الْمَرْءِ الْمُسْلِمِ السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ فِيمَا أَحَبَّ وَكَرِهَ؛ إِلَّا أَنْ يُؤْمَرَ بِمَعْصِيَةٍ، فَإِنْ أُمِرَ بِمَعْصِيَةٍ، فَلَا سَمْعَ وَلَا طَاعَةَ».
عن ابنِ عُمرَ رضي الله عنهما، أنَّ النبيَّ ﷺ قال: «عَلَى الْمَرْءِ الْمُسْلِمِ السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ فِيمَا أَحَبَّ وَكَرِهَ؛ إِلَّا أَنْ يُؤْمَرَ بِمَعْصِيَةٍ، فَإِنْ أُمِرَ بِمَعْصِيَةٍ، فَلَا سَمْعَ وَلَا طَاعَةَ».
Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume, amani iwe juu yake, amesema:
1- “Muislamu lazima asikilize amri ya Kiongozi na atii
2- Katika yale anayoyapenda na kuyachukia;
3- Isipokuwa Uasi, basi ikiwa ataamrishwa kutenda dhambi, hapo hatakiwi kusikiliza wala kutii amri”
1- Mtume, Rehema na Amani zimshukie, anauamrisha umma wake kwamba ni wajibu kuwasikiliza na kuwatii watawala, wafalme, masultani, marais na manaibu wao; Kupitia wao ndio unapatikana utulivu wa maisha na kuieneza dini na utekelezaji wa hukumu na maamrisho yake, na lau kila mtu angeruhusiwa kuasi amri ya mtawala wake, mambo yangekuwa vurugu tu, na umoja wa Waislamu ungesambaratika na ingekuwa ni rahisi kwa maadui zao kuwamaliza.
2- Sawasawa amri hiyo iwe ni katika hukumu ambazo nafsi zinatamani na zitokane na watu wanaowapenda; au katika mambo ambayo nafsi zinayachukia, hivyo subira inahitajika
Amesema Mtume Rehma na amani ziwe juu yake:
“Mwenye kuona jambo analolichukia kwa mtawala wake basi na asubiri; Kwa maana hakuna mtu anayejitoa katika umoja wa kiislamu kwa inchi moja halafu akafa, isipokuwa hufa kifo cha kijahiliyah” [1] .
3- Lakini utiifu huo si kamili; Bali umewekewa mipaka kwa yale ambayo sio maasi, ikiwa ataamrisha maasi, basi hakuna kusikia wala kutii. Akasema Mtume, amani iwe juu yake. “Utiifu ni katika kheri tu”. [2]
Na ndio maana Mwenyezi Mungu akasema:
“Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi”.
[An-Nisa: 59]
Hakusema: Watiini wenye mamlaka katika nyinyi, bali aliufanya kuwa chini ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtii Mtume Wake, amani iwe juu yake.
Ikiwa Kiongozi ataamrisha yale yanayohusisha kumuasi Mwenyezi Mungu, basi haijuzu kumtii katika uasi huu tu, si katika ukamilifu wa maamrisho na makatazo yake, na wala haijuzu kumuasi kwa hilo; Bali, imewekwa sheria kwa Muislamu kumwendea na kumnasihi kwa hekima na nasaha njema, kwa namna yoyote na inayokwenda sambamba na kila zama na hali.
1- Muislamu mwenye akili timamu hutanguliza maamrisho ya Sharia kabla ya kuangalia matamanio na maslahi yake binafsi.
2- Utiifu kwa watawala ulikuja na vidhibiti vyake katika Aya na Hadithi, kwa sababu yanapatikana maslahi ya dini na dunia, na mtu akifikiria juu ya mfumo wa nyumbani kwake, mfumo wa kazini kwake, jamii yake. atajua kuwa mambo hayawi sawa isipokuwa kuwepo watawala wa kusimamia mambo.
3- Muislamu akiona anayoyakanusha kutoka kwa mtawala wake basi afanye hima kuwaendea wenye elimu, na awaulize na awatake mawaidha, kwani pengine anaweza kudhania utiifu ni uasi, na uasi ni utiifu, na pengine hakuamiliana nao vizuri.
4- Iwapo Muislamu atabaini kuwa Kiongozi anaamrisha uasi, haijuzu kwake kumtii katika yale aliyoyaamrisha. Bali ikiwa anaweza kumnasihi amiri bila kusababisha fitnah na majaribu, atamshauri. vinginevyo hatafanya maamrisho ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
5- Haijuzu kumtii yeyote katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alitoa kiapo cha utii kwa watu kwa kumtii kwao katika wema, na yeye, amani iwe juu yake, haamrishi uasi wala haridhiki navyo, basi vipi kuhusu watu wengine?!
6- Iwapo Amiri ataamrisha maasi, hilo halimfanyi aache kuheshimiwa mojakwamoja, bali tutamtii katika jambo lisilokuwa hilo.