عن عمَّارِ بنِ ياسرٍ رضي الله عنهما قال:بَعَثَنِي رَسُولُ اللهِ ﷺ فِي حَاجَةٍ فَأَجْنَبْتُ، فَلَمْ أَجِدِ الْمَاءَ، فَتَمَرَّغْتُ فِي الصَّعِيدِ كَمَا تَمَرَّغُ الدَّابَّةُ، ثُمَّ أَتَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: «إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَقُولَ بِيَدَيْكَ هَكَذَا»، ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدَيْهِ الْأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً، ثُمَّ مَسَحَ الشِّمَالَ عَلَى الْيَمِينِ، وَظَاهِرَ كَفَّيْهِ، وَوَجْهَهُ

Kutoka kwa Ammar bin Yasir, Mungu amuwiye radhi, amesema:

1- Mtume wa Mwenyezi Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) alinituma katika jukumu fulani, nikapatwa na janaba, lakini sikupata maji, nikajibiringisha katika mchanga kama mnyama, kisha nikaenda kwa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) nikamsimulia tukio hilo. 

2- Akasema: “hakika ilikuwa inatosha kufanya kwa mikono yako hivi” kisha akapiga ardhi kwa mikono yake mpigo mmoja, kisha akapangusa mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto, na mkono wa kushoto kwa mkono wa kulia, na nje ya viganja vyake, na uso wake.

Tayammum ni ruhusa iliyowekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake pale wanapokosa maji au kushindwa kuyatumia ili kuwarahisishia, na Mtume, rehma na amani ziwe juu yake

alisema:

“Mwenyezi Mungu anapenda kutumiwa ruhsa zake kama anavyochukia kuasiwa."[1]

na Wanachuoni wameifafanua kuwa tayammam ni : kukusudia mchanga - vumbi – ili kupangusa uso na mikono kwa nia ya kuhalalikiwa  kuswali na mfano wa hayo.[2] Ni sheria iliyothibiti katika Qur’an, na Sunnah na makubaliano ya wanazuoni, na ni ruhusa maalumu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiweka katika umma huu”[3]

1. Ammar (ra) , anasimulia kuwa Mtume, (Rehma na amani ziwe juu yake) , alimtuma katika baadhi ya majukumu yake, kisha akajiotea na akapatwa na janaba, akazungusha mwili wake mzima katika mchanga safi ambao una vumbi mpaka mchanga ukaenea mwili mzima; Ili aweze kuhalalikiwa swala na kusoma Qur’an na mengine yanayofanana na hayo, kisha aliporejea kwa Mtume, rehma na amani ziwe juu yake, akamsimulia tukio zima Ili aweze kufahamu kama alifanya sawa au alikosea.

Ammar alifanya hivyo kwa sababu aliona kwamba mchanga/udongo hutumika  badala ya maji, Hivyo basi Kama maji yanavyopaswa kuenea mwili mzima katika kuosha na kujitwaharisha, hivyo hivyo ndivyo inakuwa katika tayammam kwa mtazamo wake na jitihada zake.

2.Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alimwambia kwamba ilikuwa inatosha kupiga ardhi kwa mikono yake mara moja, kisha kupangusa mikono na uso wake, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: " Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu" .

MAFUNDISHO :

  1. Kitendo cha Ammar Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake  kinaashiria kwamba ni wajibu kwa Muislamu asipofahamu hukumu mojawapo ya masuala fulani, ambayo hajui hukumu yake wala kauli ya wanazuoni katika hilo, na muda wa kumuuliza mtu mwingine ukawa hautoshi au yuko safarini na asiweze kupata fat-wa; basi wakati huo inabidi kujitahidi kadiri awezavyo, kisha ikiwa atampata wa kumuuliza, ili kujua hukumu sahihi ya kisheria juu ya suala hilo basi afanye hivyo.

  2. Katika hadithi hii inaashiria kuwa mwenye kujitahidi na kufasiri maana, ikiwa atakuwa miongoni mwa watu waliokidhi vigezo vya ijtihadi na akafasiri maana ya masuala Fulani, akawa amepatia sehemu na kukosea sehemu nyingine, basi si lazima kurudia kitendo hicho, kwani Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) hakumuamuru Ammar arudie; Kwa sababu alikosea katika sheria lakini alijitahidi, lakini alifanya twahara kwa namna isiyozingatiwa.[4]

  3. Hadithi hii inaashiria kuwa sheria ya Uislamu ina kheri nyingi na wepesi, kwani haimtwiki mtu asiyoweza kufanya, ndio maana ikaruhusu tayammam, na kuridhika na kupangusa mikono na uso.

references

  1. Imepokewa na Ahmad (5866).
  2. "Nail al-Awtar" cha al-Shawkani (1/319).
  3. "Nail al-Awtar" cha al-Shawkani (1/319).
  4. "'Iikmal Almuealim Bifawayid Muslimin"cha Qadi Iyadh (2/223).

Miradi ya Hadithi