عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى النَّبِيِّ ﷺ، وَعَقَلْتُ نَاقَتِي بِالْبَابِ، فَأَتَاهُ نَاسٌ مِنْ بَنِي تَمِيمٍ فَقَالَ: «اقْبَلُوا البُشْرَى يَا بَنِي تَمِيمٍ»، قَالُوا: قَدْ بَشَّرْتَنَا فَأَعْطِنَا، مَرَّتَيْنِ، ثُمَّ دَخَلَ عَلَيْهِ نَاسٌ مِنْ أَهْلِ اليَمَنِ، فَقَالَ: «اقْبَلُوا البُشْرَى يَا أَهْلَ اليَمَنِ، إِذْ لَمْ يَقْبَلْهَا بَنُو تَمِيمٍ»، قَالُوا: قَدْ قَبِلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالُوا: جِئْنَاكَ نَسْأَلُكَ عَنْ هَذَا الأَمْرِ. قَالَ: «كَانَ اللَّهُ وَلَمْ يَكُنْ شَيْءٌ غَيْرُهُ، وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى المَاءِ، وَكَتَبَ فِي الذِّكْرِ كُلَّ شَيْءٍ، وَخَلَقَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ» فَنَادَى مُنَادٍ: ذَهَبَتْ نَاقَتُكَ يَا بْنَ الحُصَيْنِ، فَانْطَلَقْتُ، فَإِذَا هِيَ يَقْطَعُ دُونَهَا السَّرَابُ، فَوَاللَّهِ لَوَدِدْتُ أَنِّي كُنْتُ تَرَكْتُهَا.

Kutoka kwa Imran bin Huswein, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesema

Niliingia kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) nikamuacha ngamia wangu mlangoni.Wakamjia Mtume baadhi ya watu katika familia ya Tamim, akawaambia: “pokeeni bishara enyi familia ya Tamim.”Wakasema familia ya Tamim: Umetubashiria, basi tupe mara mbili.Kisha wakaingia baadhi ya watu wa Yemen, Mtume akasema: pokeeni Bishara enyi watu wa Yemen, kwani familia ya Tamim hawakuikubali”.Wakasema watu wa Yemen: Tumeikubali, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.Wakasema watu wa Yemen: Tumekuja kukuuliza kuhusu hili jambo (la Uislamu).Akasema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Mwenyezi Mungu alikuwepo, wakati hakuna chochote kilicho kuwepo ispokuwa yeye.Na Kiti chake cha enzi kilikuwa juu ya maji.Na akaandika katika kitabu kila kitu.Na akaumba mbingu na ardhi”.Akaita Muitaji akasema: Ngamia wako ametoweka, ewe Ibn al-Huswein, basi nikaondoka mbio nikimtafuta, Ghafla nikamuona akitokomea kwa umbali.Wallahi, nikatamani laiti ningemuacha”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Ni Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji”

[Hud: 7].

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

“Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika Kitabu chenye kubainisha”

[Yasin: 12].

Mwenyezi Mungu amesema:

“Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote (9) Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza (10) Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu (11) Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua”

[Fussilat: 9-12].

Amesema Mwenyezi Mungu:

“Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo”

[Al Qamar: 49]

Miradi ya Hadithi