عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ - رضي الله عنه - أَنَّ رَسُولَ اللهِ قَالَ: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَإِذَا طَلَعَتْ مِنْ مَغْرِبِهَا، آمَنَ النَّاسُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ، فَيَوْمَئِذٍ ﴿لَا يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا﴾ [الأنعام: 158]».

Kutoka kwa Abu Hurayrah-Mwenyezi Mungu amuwiye radhi - kwamba Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:

Kiyama hakitasimama mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.Litakapo chomoza kutoka magharibi watu wote wataamini kwa pamoja.Siku hiyo: “kuamini hakutomfaa mtu chochote, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake”. [Al-An’am: 158]

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Mwenyezi Mungu amesema:

“Hakuna wanacho subiri isipokuwa wawaijie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au ziwafike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini wakati huo hakutomfaa mtu chochote, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema ewe Muhammad: Ngojeni, nasi pia tunangoja”

[Al-An'am: 158].

Na amesema Mwenyezi Mungu

“Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwisha iona adhabu yetu”

[Ghafir: 85]

Miradi ya Hadithi