عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ «مَنْ كَانَتْ لَهُ مَظْلِمَةٌ لِأَخِيهِ مِنْ عِرْضِهِ أَوْ شَيْءٍ، فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ اليَوْمَ، قَبْلَ أَنْ لاَ يَكُونَ دِينَارٌ وَلاَ دِرْهَمٌ، إِنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ، أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلِمَتِهِ، وَإِنْ لَمْ تَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ، أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ، فَحُمِلَ عَلَيْهِ».

Kutoka kwa Abu Hurayra, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie.

1- “Atakayekuwa na dhulma kwa ndugu yake, heshima yake au kitu chochote kile, basi na amrudishie hayo leo kabla ya siku ambayo haitakubaliwa dinari wala dirham. 

2- Akiwa na kheri itachukuliwa kutoka kwake kwa kiasi cha dhulma yake, na ikiwa hana amali njema itachukuliwa baadhi ya maovu ya aliyeifanyiwa dhulma na kubebeshwa”.

Muhtasari wa Maana

Ni lazima mtu arudishe mali za dhulma kwa wanaostahiki, na awaombe msamaha waliowadhulumu, kabla ya kuadhibiwa kwa matendo mema na mabaya.

Miradi ya Hadithi