31 - MIONGONI MWA AINA ZA MAKADIRIO YALIYOTANGULIA

عن عبدِ الله بنِ مسعودٍ قال: حدَّثنا رسولُ الله ﷺ- وهو الصادقُ المصدوقُ -: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَبْعَثُ اللهُ إِلَيْهِ مَلَكًا بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ، فَيُكْتَبُ عَمَلُهُ، وَأَجَلُهُ، وَرِزْقُهُ، وَشَقِيٌّ أَمْ سَعِيدٌ، ثُمَّ يُنْفَخُ فِيهِ الرُّوحُ، فَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ، حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ، فَيَدْخُلُ الجَنَّةَ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ، حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَاإلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ، فَيَدْخُلُ النَّارَ» متفق عليه



Kutoka kwa Abdullah bun Masood, amesema: alitwambia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) – na yeye ndiye mkweli anae kubalika -

1.Hakika mmoja wenu hukaa katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha anakuwa pande la damu kwa siku nyinge kama hizo, kisha anakuwa pande la nyama kwa siku nyingine kama hizo 2.Kisha Mwenyezi Mungu anamtuma malaika kwa ajili ya mambo manne, aandike matendo yake, kifo chake, riziki yake na atakuwa mwema au muovu 3.Kisha anapuliziwa roho. 4.Kwa hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Motoni mpaka inabaki baina yake na kuingia Motoni kiasi cha dhiraa urefu wa mkono kutoka kwenye kiganja mpaka kwenye kiwiko, mipango ya Mwenyezi Mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Peponi, aningia Peponi. 5.Na hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi mpaka inabaki baina yake na kuingia Peponi kiasi cha dhiraa, mipango ya mwenyezi mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Motoni, anaingia Motoni” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu.




Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

12. " Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. 13. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. 14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. 15. Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. 16. Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa ". 

[muuminuun: 12-16]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

7." Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. 8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. 9. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru. "

[Al-Sajdah: 7-9]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

" Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu. "

[Al-Isra: 85]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

11. "Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi. "

[Hajj: 11]

" Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu  Na jengo lao hilo walilo lijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima."

[At-Tawbah: 115]

Miradi ya Hadithi