20 - NAFASI YA MASWAHABA RADHI ZA MWENYEZI MUNGU ZIWAFIKIE

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «لَا تَسُبُّوا أَصْحَابِي، لَا تَسُبُّوا أَصْحَابِي، فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ أَنْفَقَ مِثْلَ أُحُدٍ ذَهَبًا، مَا أَدْرَكَ مُدَّ أَحَدِهِمْ، وَلَا نَصِيفَهُ».

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam."Msiwatukane Maswahaba zangu, Msiwatukane Maswahaba zangu,Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, kama mmoja wenu akitoa dhahabu kama sawa na Mlima wa uhudi, basi hatafikia gao la mmoja wao, wala nusu yake.

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amekataza umma wake kuwatukana maswahaba zake. Kwani wao - kwa ukubwa wa walichoupa Uislamu – ni watu wenye malipo makubwa.

Miradi ya Hadithi