عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ ﷺ يَقُولُ: «ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ: مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا»
عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ ﷺ يَقُولُ: «ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ: مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا»
Kutoka kwa al-Abbas ibn Abd al-Muttalib
(Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) akisema: 1.“Ameipata ladha ya imani. 2. Aliyemridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi 3. Na Uislamu kuwa Dini aliyoichagua. 4. Na Muhammad kuwa ndio Mtume wa haki”
Al-Abbas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, anasimulia kutoka Kwa Mtume (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) akisema:
Imani ina ladha na utamu, na Mtume (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) alitumia neno “ameonja” ingawa si kimininika wala si chakula, katika kuwakilisha maana yake; kwani Iwapo mtu ataonja chakula na kinywaji na akahisi ladha, basi pia anahisi athari ya Imani katika nafsi mtu ambaye imaan imemuingia na kukita katika nasi yake.[1]Na Miongoni mwa maana ya ladha hii ni kufunguka kwa moyo, na utulivu wa akili, na kuwa na raha ukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu, hivyo mtu anakuwa hapendelei madhambi bali anajiepusha nayo, na kufanya mambo ya faradhi kwake inakuwa vyepesi, hali hii inamfanya kuvumilia tabu zote, wala hakati tamaa na Rehema za Mola wake Mlezi bali huridhika na makadirio yake juu yake, na ladha hii nzuri na tamu haipatikani ila kwa masharti.
2. Sharti la kwanza ni kuridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio Mola Mlezi, na kuridhika maana yake ni: kukinaika na kitu na kutosheka nacho dhidi ya kitu kingine, na kutosheka na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuamini habari zake, na kusalimu amri kwake, na kuwa na subira na kujipa moyo katika hukumu Zake za makakadiro yake.Na kuridhika hapa hakukusudii kukiri uwepo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani kukiri uwepo wake ni sharti la msingi katika Uislamu, lakini kinachokusudiwa ni kuridhika maalumu, ambako ni kuridhika Mwenyezi Mungu kuwa ndio Mtawala katika Maisha yake, na Muumba, mwenye kumuwekea sheria, na ameridhika na hukumu zake na kuridhia sheria yake, hivyo anamuabudu, anampenda, anamkubali, anamtegemea na ni muaminifu kwake, na hakuna mwingine anayeogopa woga wa siri tofauti na yeye, na kuridhika katika hukumu yake na makadirio yake. Na mtu huyo hafanyi lolote la kumkasirisha Mola Mlezi.[2]
3. Sharti la pili: kuridhia Uislamu kuwa ndio dini ya kweli, na hii ina maana ya kukubaliwa kisheria; hivyo basi anafuata maamrisho na kuacha makatazo, na amechagua Uislamu juu ya dini zote, na akaufanya kuwa nguzo yake imara ambayo ndio kimbilio na tegemeo lake, ambalo anapenda na kuchukia kwa misingi ya dini hiyo, na yupo tayari kutoa sadaka na kila chenye thamani ya kwa ajili yake.
4. Sharti ya tatu: kuridhia kwamba Muhammad (rehma na amani zimshukie) ni Nabii wa kweli aliyetumwa, na hii ni pamoja na kuamini kuwa yeye ni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuyakubali aliyoyaleta kutoka kwa Mwenyezi Mungu, katika maamrisho na makatazo, na kuikubali Sheria hiyo, na kuithibitisha, na kutenda na kusalimu amri. Na kuridhika kwa wapenzi wanaomfuata, na wanaoongozwa na muongozo wake, na wanaomuiga, wanaofuata utiifu wake, na wanaojitolea maisha yao na vitu vyao vya thamani kwa ajili ya kulinda mienendo yake, na wanashauku ya kukutana naye.Hii inaonyesha kwamba hakuna mtu anayekuja na dhana ya imani isipokuwa ana misingi mitatu ya dini. Kumuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake na dini yake.
Al-Abbas bin Abdul-Muttalib, alimuamini mtoto wa ndugu yake, japo kuwa alikuwa mkubwa kuliko yeye, na kwa sababu hiyo alivumilia maudhi na uadui wa watu wake na familia yake, na hili ni tabia inayomsukuma mtu mwenye akili timamu. kukubali ukweli kutoka kwa mtu yeyote, awe Mkubwa au mdogo, na awe mwenye nguvu au dhaifu, tajiri au maskini.
Al-Abbas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alithibiti pamoja na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) wakati masahaba zake wengi walipokimbia siku ya vita vya Hunayn. Hii inaashiria ukweli wa Uislamu wake na kuipata ladha ya Imani licha ya kuwa alikuwa mgeni katika uislamu (yaan hakuwa na siku nyingi ameingia katika uislamu). Sasa inakuwa vipi kwa mtu aliyezaliwa katika Uislamu au amekaa ndani yake kwa miaka mingi na bado anamuabudu Mungu kwa kutegea?! tujitahidi kuthibitisha Imani katika vifua vyetu., ili tuwe kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Miongoni mwa Waumini wapo watu wanaotimiza ahadi zao kwa Mwenyezi Mungu”
[Al-Ahzab: 23].
Imani ina ladha ambayo hawezi kuitambua mtu aliyeishi katika imani hiyo kwa muda kwa sababu hatambui uhalisia wake, au hakuhisi thamani yake na vitu vingine. Basi Kila unapojiona unapendelea starehe za dunia kuliko starehe za imani, ikumbushe nafsi yako na ihimize kutafuta ladha ya Imani.
Tafuteni radhi Radhi za Mwenyezi Mungu kwa kukumbuka kuwa Yeye ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, Mjuzi wa yote, na sifa zake nyinginezo ambazo ndani yake nafsi hutulia kwa kuamini habari zake, na kusalimu amri kwa kufuata maamrisho na kuacha makatazo Yake, na kutulizana juu ya makadirio yake, na kwa kukumbuka neema zake za wazi na zilizofichikana, na kwamba yale tuliyokuwa hatuyajui katika neema zake ni makubwa zaidi. Na yale tuliyokuwa hatuyajui kuhusu uumbaji wake na hekima yake katika kuyasimamia ni makubwa kuliko tunayoyajua.
Ridhika na Uislamu kuwa ndio dini kwa kujua kuwa ni sheria ya Mwenyezi Mungu, ambayo hakuna mjuzi Zaidi yake, wala mwenye hekima kuliko yeye, wala hakuna mwenye huruma kuliko Mwenyezi Mungu, na kwamba mwenye Akili anajua ukamilifu wake wa wazi kiasi ambacho kinamtosha kuridhia yote asiyoyajua.
Tosheka kuwa Nabii Muhammad ndio Mtume wako, kwa kukumbuka ukamilifu wake katika kila tabia za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na utimilifu wa elimu na akili yake, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu juu yake na kuhifadhiwa kwake. kumbuka kujitoa muhanga kwa ajili ya ummah wake, na huruma yake kwao, na kwamba akilinganishwa Mtume na watu wengine, mapungufu ya viumbe vyote yatadhihirika mbele ya Mtume (Rehma na Amani zimshukie).
Dunia hii, licha ya dhiki, uchovu na dhuluma ziliyomo ndani yake, inakuwa ni pepo kwa Muumini kwa kule tu kuridhika, kunyenyekea na Kuamani, ndio maana ikasemwa: “Kuridhika ni Pepo ya Duniani, na starehe kwa wanaojua”. Hivyo basi tunaweza kuingia katika pepo na bustani yetu duniani kwa kuridhika! Muislamu akipatwa na msiba au akakosa mlango wa riziki na kheri, anasalimisha amri yake kwa Mola wake mlezi, na anaamini kuwa hakuna litakalotupata isipokuwa lile aliyotuandikia Mwenyezi Mungu litupate. Na hapo muumini anahisi utuilivu, na anasalimika kutokana na kukata tamaa kwa aliyoyakosa.
Amiri wa waumini, Omar bin Abdul Aziz, alikuwa akiomba dua hii: “Ewe Mola wangu niridhishe kwa amri yako, na unibariki katika kudra yako, niepushe kupenda kuharakisha ulichochelewesha, wala kuchelewesha ulichoharakisha”[3].
Aliulizwa Yahya bin Muadh: Ni lini mja anafikia Daraja la kuridhika? Akasema: Akisimama katika misingi minne katika yale anayomridhisha Mola wake, kwa kusema akimwambia Mola wake: ewe mola wangu Ukinipa napokea, na ukininyima naridhika, na Ukiniacha nazidhisha kukuabudu, na ukiniita nakuitikia[4]). Ni lazima tujichunguze wenyewe; Je, tuna sifa hizi? Kwa kadiri tulivyo na sifa, tumefikia daraja la kuridhika.
Amesema Mshairi:Kuridhika kwako ni bora kuliko Dunia na vilivyomo,,,,, Ewe mwenye kuimiliki nafsi, idhibiti na uiweke karibu.Roho haiwezi kukamilisha matarajio yake,,,,, bila ridhaa yako hata kidogo.Kunitazama kwako ewe ninayekuomba na kukutarajia,,,,,, ni bora kwangu kuliko dunia na vilivyomo.