عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ:«الإِيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ - أَوْ: بِضْعٌ وَسِتُّونَ - شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإِيمَانِ» متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimfikie):“Imani ina daraja sabini na kitu, au sitini na kitu.Daraja bora zaidi ni kusema: Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu.Na daraja la chini kabisa ni kuondoa maudhi njiani.Na haya (aibu) ni daraja katika daraja za Imani.” Hadithi hii Imepokelewa na Imam Bukhari Na Muslimu.

Imepokewa na Al-Bukhari (9) na Muslim (35),

Muhtasari wa Maana

NI: Abu Huraira, Abd al-Rahman ibn Sakhr al-Dawsi, al-Azdi, alisilimu mwaka wa saba. amesema Ibn Abi Dawood: “Watu wa Hadith wamekubaliana kuwa Abu Hurairah ni katika maswahaba waliopokea hadithi nyingi.” Aliwahi kuwa kiongozi katika baadhi ya tawala, alifariki katika mji wa Madina mwaka wa (58 AH

Miradi ya Hadithi