عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ يَقُولُ: «جَعَلَ اللهُ الرَّحمةَ في مِائَةِ جُزْءٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ جُزْءًا، وَأَنْزَلَ فِي الأرْضِ جُزْءًا وَاحِدًا، فَمِنْ ذَلِكَ الجُزْءِ يَتَرَاحَمُ الخَلْقُ، حَتَّى تَرْفَعَ الفَرَسُ حَافِرَهَا عَنْ وَلَدِهَا؛ خَشْيَةَ أَنْ تُصِيبَهُ» متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma Na Amani Zimshukie) akisema:

1. “Mungu amejalia huruma katika mafungu mia moja, 

2. kisha akabakiza kwake sehemu tisini na tisa (za huruma) na akateremsha ardhini sehemu moja tu. 

3. Kutokana na sehemu hiyo viumbe uhurumiana, (kiasi kwamba) farasi hunyanyua kwato yake kwa mtoto wake kwa kuogopea asimkanyage) .” imepokelewa na Bukhari Na Muslim .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴾Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu﴿.)

[Al'aneam: 54]

Amesema Mwenyezi Mungu Mutuku:

﴾Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema﴿.

[Al-A'raf: 56]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia:

﴾Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mcha Mungu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu﴿, .

[Al-A'raf: 156]

Miradi ya Hadithi