عن أبي هريرة : أنَّ رَجُلًا قالَ للنبيِّ ﷺ: أوْصِنِي، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ»، فَرَدَّدَ مِرَارًا، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ».

Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

1- Mtu mmoja alimwambia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Ninasihi. 

2- Akasema Mtume: “Usikasirike” 

3- Mtume alirudia mara kadhaa akisema: “Usikasirike”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu :

“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamungu (133) Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema”

[Al Imran: 133, 134]

Na Amesema Mwenyezi Mungu:

“Basi vyote mlivyo pewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu kwa ajili ya walio amini, na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi (36) Na wanao yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao husamehe”.

[Al-Shura: 36, 37]

Miradi ya Hadithi