عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله ﷺ فقال: يا رسول الله، من أحق الناس بحسن صحابتي؟ قال: (أمُّك) قال: ثم من؟ قال: (أمك)، قال: ثم من؟ قال: (أمك)، قال: ثم من؟ قال: (أبوك)، وفي رواية قال: (أمك، ثم أمك، ثم أمك، ثم أباك، ثم أدناك أدناك)



Kwa kutoka kwa Abu Huraira, Allah amuwiye radhi, amesema:

1. Alikuja mtu kwa Mtume rehma na amani zimshukie na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani katika watu anastahiki zaidi usuhuba wangu? 2. Akasema Mtume: (Mama yako) Akasema: Kisha nani? Akasema: (Mama yako), akasema: Kisha nani? Akasema: (mama yako) 3. Akasema: Kisha nani? Akasema Mtume: (Baba yako), na katika riwaya akasema: (Mama yako, kisha mama yako, kisha mama yako, kisha baba yako, 4. Kisha anafuatia aliye karibu yako”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri” .

[Al-Baqara: 215]

Na akasema Allah aliyetakasika: “Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba  yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini”

[Al-Ahqaf: 15]

. Mwenyezi Mungu utukufu ni wake amesema: “Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima (23) Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni”

[Al-Isra: 23, 24].

Miradi ya Hadithi